HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 23 October 2018

AFISA MAHUSIANO AMPONGEZA DIWANI KATA YA MAJI CHUMVI TABATA KWA JUHUDI ZA MAENDELEO

Na Khadija Seif, Globu ya Jamii
Afisa Mahusiano Halmashauri Wilaya ya Ilala Tabu Shaibu amepongeza juhudi za Diwani wa kata ya Kisukulu kwa kukarabati miundo mbinu bila ya kusubiri serikali.

Tabu ametoa pongezi hizo baada ya diwani huyo kutekeleza kazi za kurekebisha  baadhi ya barabara ambapo pengine zingesubiri mpaka serikali ifanye marekebisho hayo ila ameweza kukusanya vijana na kutengeneza barabara hiyo.

Barabara hiyo imekuwa ni njia kubwa ya watu kutoka maeneo ya Gongo la mboto,Bonyokwa,Tabata pamoja na Ubungo.

Tabu  ameeleza kuwa serikali inaendelea na utaratibu ambao ulishapangwa kwa kila sehemu korofi za barabara kurekebishwa kwa awamu na mpaka sasa kuna greda mbili ambapo moja liko Kwenye ukarabati na hivyo kwa barabara hiyo kuendelea kusubiri kwa muda.


Amewaomba wananchi waendelee kushirikiana kikamilifu na diwani huyo katika kuboresha maendeleo ya kata hiyo kwani biashara zinazofanywa na wakazi nyingne huhitaji Miundombinu ambayo itawezesha biashara kuwafikia wateja kwa haraka zaidi muhimili mkuu ukiwa ni Barabara.

Diwani wa Kata ya Maji Chumvi Tabata,  Joseph Sayenda ameshirikiana na Wananchi wa kata hiyo katika kuboresha Miundombinu ya awali ya barabara ambayo kwa miaka mingi imekua tatizo kwa Wakazi hao.

Sayenda amesema wananchi wa kata ya maji chumvi waliiona adha hiyo kwa muda mrefu na kuona fursa ya kushirikiana kukarabati barabara hiyo huku wakiendelea kusubiri serikali kutatua tatizo hilo.

Amefafanua kuwa Katika kuunga mkono rai ya serikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt  John Pombe Magufuli Katika kuendeleza Tanzania ya viwanda nchini ambapo katika barabara Hiyo kuna kiwanda cha mashine ya kusaga nafaka ambapo wakazi hutumia kwa ajili ya shughuli za kila siku.

Wananchi wa kata ya  Maji Chumvi Tabata wakifanya ukaraati wa barabara inayounganisha maeneo ya Gongo la mboto,Bonyokwa,Tabata pamoja na Ubungo.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad