HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 23, 2018

WAZIRI MKUU AITAKA SIDO KUBUNI TEKNOLOJIA RAFIKI

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Maonesho ya Shirika la  Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) kwenye uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu, Oktoba 23, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Badhi ya wananchi wa  mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kufungua Maonesho ya Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO)  kwenye uwanja wa Nyakabindi.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) kitanzania ili wakue na kuwa wawekezaji wakubwa. Pia kuwawekea mazingira wezeshi ya kufanya shughuli zao.”
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama chaki zilizotengenezwa wilayani Maswa katika maonesho ya Shirika la Kuhudumia  Viwanda Vidogo (SIDO) kwenye  uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu, Oktoba 23, 2018 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea jembe la asili kutoka mhunzi,  Mashaka Daniel wa  Bukoba katika Maonesho ya Shirika la Kuhudumia  Viwanda Vidogo (SIDO)  aliyoyafungua kwenye uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu, Oktoba 23, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Ofisa wa  Ufundi wa Shirika la Kuhudumia  Viwanda Vidogo (SIDO), Prosper Godfrey (kulia)  kuhusu majiko makubwa yanayotengenezwa na SIDO wakati alipofungua Maonesho ya SIDO kwenye uwanja wa Nyakabindi  mkoani Simiyu Oktoba  23, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simyu, Anthony Mtaka na watatu kushoto ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi  Stella Manyanya.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka wakitazama asali ya Pinda katika maonesho ya Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo(SIDO) kwenye uwanja wa Nyakabindi mkoani Simuyu, Oktoba 23, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiandika katika ubao kwa kutumia chaki zilizotengenezwa wilayani Maswa mkoani  Simiyu katika Maonesho ya Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo  (SIDO) aliyoyafungua kwenye uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu, Oktoba 23, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameliagiza Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO)lijielekezekatika kubuni teknolojia na mitambo rafiki inayolenga kutatua changamoto za wajasiriamali kulingana na mazingira yao. 

Amesema Serikali inaendelea kuimarisha shughuli za SIDO lakini bado kuna  changamoto za wajasiriamali wadogo ambazo lazima zishughulikiwe kwa kasi kubwa ili kufungamanisha shughuli za SIDO na uchumi wa Viwanda

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Oktoba 23, 2018) wakati akifungua Maonesho ya SIDO kitaifa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Nyakabindi vilivyoko wilayani Bariadi mkoani Simiyu na kuhudhuriwa na wajasiriamali 500.

Amesema ili kufikia uchumi wa kati inambidi kila Mtanzania mahali alipo afanye kazi kwa bidii, maarifa na ubunifu. “Tusipoteze wakati kwa kufanya mambo yasiyo na tija. Tuzingatie falsafa ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Hapa Kazi Tu.”

“Mfano kwa hapa Bariadi, tunatarajia SIDO watuletee teknolojia na mitambo inayoweza kurahisisha ukamuaji wa mafuta yanayotokana na mbegu za alizeti na pamba, kwa Dodoma taknolojia na mitambo kwa ajili ya kuchakata zabibu.”

“Kigoma pelekeni teknolojia na mitambo kwa ajili ya kuchakata mbegu za michikichi na kwenye maeneo yanayolimwa korosho teknolojia na mitambo  ya kubangua korosho na maeneo kama Ilula ambayo yanazalisha nyanya kwa wingi wapate teknolojia na mitambo ya kusindika na kuhifadhi nyanya na mbogamboga.” 

Waziri Mkuu amesema ili nchi iweze kupata mafanikio, SIDO inatakiwa iwaunganishe wajasiriamali na taasisi mbalimbali za fedha ili wapate mikopo yenye masharti nafuu. “Mahitaji ni makubwa hivyo lazima SIDO ishirikiane na taasisi nyingine ikiwemo Baraza la uwezehaji Wananchi Kiuchumi. (NEEC).”

Pia, Waziri Mkuu amewasihi wajasiriamali wanaoshiriki maonesho hayo kutumia fursa hiyo kujifunza namna nzuri ya kuboresha viwango vya bidhaa zao na kubadilishana ujuzi na uzoefu, kupanua masoko na kubaini teknolojia zitakazorahisisha uzalishaji wa bidhaa. 

‘’Kumbukeni kuwa Serikali ina matarajio makubwa katika sekta ya viwaanda hususan katika kuiwezesha nchi kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.’’ 

Awali, Waziri Mkuu alitembelea mabanda mbalimbali ya washirii wa maonesho hayo yakiwemo ya taasisi za Serikali zinazotoa huduma katika sekta ya viwanda na biashara zikiwemo Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO); Shirika la Viwango Tanzania  (TBS) 

Mamlaka ya Vyakula na Dawa (TFDA), Wakala wa Vipimo (WMA); Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan-Trade); Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na Balaza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC). 

Waziri Mkuu ametoa wito kwa taasisi hizo zikikishe zinafanya kazi kwa kushirikiana, ujuzi na weledi mkubwa katika kuwawezesha wafanyabiashara wadogo kuendesha shughuli zao kwa viwango vinavyotakiwa. 
“Jukumu la mamlaka za Serikali ni kufundisha, kuwalea na kuwaelekeza wajasiriamali wa kitanzania ili wakue na kuwa wawekezaji wakubwa. Pia kuwawekea mazingira wezeshi ya kufanya shughuli zao.”

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad