HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 7 September 2018

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO WASAINI MKATABA WA MKOPO WENYE RIBA ZIRO

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
WIZARA ya Fedha na mipango kwa niaba ya serikali imesaini mkataba Mkopo wa fedha kati ya serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na benki kuu ya dunia jijini Dar es salaam leo kwaajili ya kusafirisha, kuzalisha na kusambaza nishati ya umeme na maji.

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wizara ya fedha na Mipango, Dotto James amesema kuwa mkataba huu wa mkopo huu utahusisha usambazaji wa maji katika maeneo ya vijijini katika mikoa 17 ya Tanzania pamoja na umeme. Pia Katibu Mkuu wizara ya fedha na mipango amewashukuru benki ya dunia kwa kutoa mkopo usio na riba kabisa.

Mkopo huo kutoka Benki ya dunia kiasi cha shilingi trilioni 1.04 ambapo itatumika katika mradi wa umeme na maji kwa mikoa ya kusini ambayo ni  Iringa Kisada,Tunduma, Mbeya hadi mpaka wa Zambia.

Nae Katibu Mkuu wizara ya Maji safi na maji taka, Kitila Mkumbo amesema kuwa fedha hizo zitatumika kikamilifu katika lengo lililopangwa na serikali kwa mikoa 17 katika usambazaji wa maji maeneo ya vijijini.

Kwa upande wa Katibu Mtendaji uwekezaji wizara ya Nishati na Madini, Khalid James amesema kuwa kwa upande wa Nishati ya umeme wataweza kuunganisha gridi ya Taifa kwa mikoa ambayo haijafikiwa na gridi ya taifa.
Katibu Mkuu wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 7,2018 kabla ya kusaini Mkataba wa mkopo wa fedha kwaajili ya usambazaji wa maji vijijini na uboreshaji, utengenezaji na kuzalisha umeme hapa nchini.
 Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bella Bird akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Septemba7, 2018 kabla ya kusaini Mkataba wa Mkopo wenye masharti nafuu pamoja na riba zero ambapo mkopo huo utakuwa kwaajili ya kutekeleza mradi wa maji vijijini pamoja na umeme.
 Katibu Mkuu wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James (Kulia) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bella Bird (Kushoto) wakisaini Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu na wenye riba ziro kwaajili ya uboreshaji na utengenezaji mifumo ya umeme na maji katika maeneo ya vijijini hapa nchi.
  Katibu Mkuu wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James (Kulia) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bella Bird (Kushoto) wakibadilishana Mkataba wa mkopo jijini Dar es Salaam leo, Septemba 7,2018 wenye masharti nafuu na wenye riba ziro kwaajili ya uboreshaji na utengenezaji mifumo ya umeme na maji katika maeneo ya vijijini hapa nchi.
 Katibu Mkuu wa wizara ya maji safi na maji taka (DAWASO), Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusu mpango waliojiwekea katika kuboresha na kusambaza maji hapa nchini katika maeneo ya vijijini. Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bella Bird.
Kaimu Mkurugezi mtendaji- Uwekezaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Khalid James kulia akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya katibu Mkuu wizara ya fedha na Mipango kusaini mkataba wa Mkopo wa fedha kwaajili ya uboreshaji na usambazaji wa maji pamoja na umeme.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad