HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 17 September 2018

WAZIRI MBARAWA AFUNGUA MRADI WA MAJI WA KIWALANI LEO JIJINI DAR

*Awataka Dawasa wawaunganishie maji wananchi walipe kidogo kiodogo

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa amezindua mradi wa maji wa Kiwalani  na kuwataka Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasa) kuhakikisha wanawaunganishia wananchi wa eneo hilo maji kwa mkataba ili walipe kidogo kidogo kwakuwa serikali imetumia fedha nyingi sana kufanikisha mradi huona Malengo ya Serikali ni kuona watanzania wanapata maji kwa asilimia 90.


Amezungumza hayo wakati wa uzinduzi wa mradi huo uliokuwa umekamilika tayari na wananchi wa Kiwalani wakianza kupata maji safi na salama kuitia vizimba vitano vilivyokuwa vimeshajengwa tayari.


Profesa Mbarawa amesema, kumalizika kwa mradi huu ni moja ya ahadi ya serikali ya kuhakikisha kila mwananchi na eneo la Kiwalani wana zaidi ya miaka 30 hawajawahi kuwa na maji safi ya Dawasa  na wamekuwa wanatumia  chumvi katika kipindi chote hicho.

Amesema Profesa Mbarawa, ukiachana na mradi huo mpaka sasa serikali bado ina miradi mingine ikiwamo mradi wa Bilioni  133.2 ambao ni mradi wa kutoka Benki ya dunia na maji yatakayozalishwa hapo yatapatikana maeneo ya Dar es Salaam na Bagamoyo.

Amesema, Mradi mwingine ni wa Usambazaji maji wa Kiluvya, Salasala, Kimara na Goba utakaogharimu Bil 74.46, huku akisisitiza zaidi katika miradi ukiwamo mradi wa maji taka wenye thamani ya Bil 156.64 ambao yote kwa amoja ikikamilika itahakikisha inaleta manufaa kwa wakazi wa Dar es Salaam na Pwani.

"kuna Visima 21 katika  mradi wa Kimbiji Mpera tayari vimeshakamilika  na kabla ya 2020 maji yatapatikana kwa maeneo yote ikiwamo Kigamboni ambapo kumekuwa na changamoto ya maji safi kwa muda mrefu sasa,".

Waziri Mbarawa ameeleza kuwa, anatambua kuna baadhi ya maeneo yana changamoto ya maji na baadhi ya maeneo hayo ni Gongo la Mboto, Pugu,Kinyerezi na maeneo ya karbu  na kwa namna Dawasa mpya inavyofanya kazi kwa kasi inaonesha changamoto ya maji itakuwa ni historia ndani ya Mkoa wa Dares Salaam na Pwani.

Amemalizia kwa kuwaasa wananchi kununua maji ya Dawasa yenye gharama nafuu  na kuchana kununua maji ya maboza wanayouziwa kwa ei kubwa tofauti na Dawasa anbao wanauza Unit moja sawa na  lita 1000 kwa sh 1664 na sasa kununua maji ktk magari umekwisha.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi  na Maji Taka Mkoa wa Dar es Salaam (Dawasa) Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa miradi yote itakapokamilika wakazi wa Dar es Salaam na Pwani watapata maji ya uhakika.

Luhemeja amesema kuwa, ndani ya siku 100 za Dawasa Mpya watahakikisha miradi inakamilika na mingine wakandarasi wakiingia kazini ili kufanikisha upatikanaji wa maji kwa wakazi wote na wakitimiza hitaji la kuongeza wateja wapya 200,000 kutokana na miradi hiyo  ya maji.

Pamoja na hilo, Luhemeja amesema kuwa moja ya mkakati mwingine wa Dawasa  mya ni kuona wanaongeza ukusanyaji wa mapato kwa kufikia Bilioni 12 ikiwamo kuwafuatilia wale wote wenye madeni.


Mratibu wa Mradi wa Kiwalani Mhandisi Ramadhani Mtindasi amesema kuwa mradi wa Kiwalani ni Km 13.32 ukiwa na vizimba vinane lakini mpaka sasa tayari wameshajenga vizimba vitano na karibuni watamalizia vitatu. na ukiwa umekamilika mwishoni  wa mwezi wa nane.

Amesema mradi huo mpaka sasa umeweza kuata Wateja wapya 450  na waliounganishwa ni  246 ila wakati wa ujenzi wa mradi huu waliata Changamoto kubwa sana kwa kuwa eneo hilo lina mkondo wa maji  wakati wa umewakaji mitaro mitaro 

Amemalizia kwa kusema mradi huo una awamu tatu, na tayari awamu ya kwanza na ya pili umekamilika kwa  asilimia 100 limekamilika. 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa (wapili kushoto) kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah  Kaluwa (wakwanza kushoto) wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa mradi wa maji Kiwalani Bom Bom jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Segerea,Bonnah Kaluwa wakifungua  mradi wa maji Kiwalani Bom Bom jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasa) Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza machache na kumkaribisha Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, kuzungumza  wananchi wa Kiwalani  Bom Bom leo jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame  Mbarawa, (wapili kushoto), akionyeshwa ramani ya mradi wa maji  katika kata Kiwalani Bom Bom na  Mratibu wa Mradi wa Kiwalani Mhandisi Ramadhani Mtindasi leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, akiwa ameambatana na watendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasa),wananchi wa Kiwalani Bom Bom wakielekea sehemu ya mrad wamaji.

Baadhi ya watendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasa)  
 (Picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad