HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 17, 2018

CHAMA CHA MIELEKA KUFANYA UCHAGUZI WAKE OKTOBA 27.



Baraza la mchezo la Taifa (BMT) limetangaza uchaguzi wa Viongozi wa Shirikisho la Mieleka ya Ridhaa Tanzania (TAWF) unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Oktoba, 2018 katika ukumbi wa msasani Beach Club, jijini Dar es Salaam.

Fomu zimeanza  kutolewa katika Ofisi za Baraza na pia kupatikana katika tovuti ambayo ni www.nationalsportscouncil.go.tz kuanzia tarehe leo tarehe 17 Septemba, 2018, ambapo mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni tarehe 19 Oktoba, 2018.

Aidha, usaili utafanyika tarehe 26 Oktoba kuanzia saa 3:00 asubuhi kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo siku inayofuata ha na mahali mtafahamishwa kabla ya kufika tarehe hizo.

Nafasi zinazogombewa ni;


Rais 



Makamu wa Rais





Katibu Mkuu


Katibu Msaidizi


Mhasibu Mkuu


Afisa Habari


Wajumbe watatu (3) wa kuchaguliwa












SIFA ZA WAGOMBEA;-.



.Awe mwanachama wa shirikisho la mieleka nchini (TAWF).


.Awe na umri wa kuanzia miaka 25 na kuendelea.



.Asiwe amewahi kupatikana na kosa la jinai.


.Kwa nafasi ya Rais, Makamu wa Rais, Katibu Mkuu na Msaidizi, awe na elimu ya kidato cha nne na kuendelea pamoja na uwezo wa kuandika na kusoma kingereza na Kiswahili kwa ufasaha.


.Awe na akili timamu.



.Mhasibu Mkuu na Msaidizi awe na cheti cha uhasibu, stashahada au zaidi ya hapo. 


.Sifa za wajumbe wa kamati mbalimbali wawe na uzoefu wa mchezo wa mieleka, wanaojua sheria za mchezo wa mieleka au wawe wameshawahi kuwa viongozi katika ngazi ya vilabu, wilaya, mkoa na Taifa.
.Asiwe amewahi kucheza,kuongoza au kushiriki kwa namna yoyote ile mieleka ya kulipwa.

BMT linatoa wito kwa wenye nia ya dhati ya maendeleo ya mchezo huu, kujitokeza kuchukua fomu na kugombea nafasi stahiki ili kuendeleza shirikisho pamoja na kuiletea sifa nchi. 

Fomu zilipiwe katika Akaunti ya Baraza kwa jina la National Sports Council Ac. No. 20401100013 na kuwasilishwa risiti iliyolipiwa Benki pamoja fomu zilizojazwa kwa usahihi.






Kwa wa rais na makamu wake 
Ada ya fomu ni sh. 50,000/= na kwa nafasi zingine zilizisalia 

Ada ya fomu itakuwa ni sh. 30,000/

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad