HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, September 29, 2018

WANANCHI 40,000 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI WA SALASALA


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) imeunda kikosi maalum cha kufanya kazi ya maunganisho mapya ili kuongeza wateja wa maji. 



Kazi hii imeanza leo rasmi katika eneo la Salasala ikiwa inaongozwa na Mhandisi Mtindasi chini ya Mkurugenzi wa Huduma Kwa Wateja Ritamary Lwabulinda. 


Mradi huo wa Salasala utawanufaisha wananchi 40,000 wa maeneo hayo ikiwa ni katika kutekeleza siku 100 za DAWASA mpya.
Katika kuhakikisha kuwa kazi inafanywa kwa weledi na usimamizi wa kutosha mhandisi Mtindasi atasaidiwa na wahandisi wengine 3 na mafundi 3 na vijana 150 kutoka Veta.
Mradi huo utakuwa na awamu tofauti na katika awamu ya kwanza imeweza kuhusisha vijana 50 ambao tayari wamemaliza mafunzo na leo hii tayari wapo kazini. 
Wananchi wanaoishi eneo la Salasala watafaidika moja kwa moja na mradi huo na ndio wataanza kufanyiwa maunganisho kwani tayari kuna mtandao na maji kutoka mtambo wa Ruvu Chini yataunganishwa hivi karibuni.

Aidha katika mikoa mingine ya kazi ya DAWASA kuna miradi midogo midogo ya kusogeza huduma kwa wateja inayoendelea. Miradi hii yote inagharamiwa na DAWASA na wateja wataunganishiwa maji kwa mkopo.
 


Wataalam kutoka Mamlaka ya Maji wanaendelea kufanya 'survey' kwenye maeneo mbalimbali ya mradi kuweza kubaini maeneo ya maunganisho mapya kwa ajili ya kusogeza huduma ya maji kwa kila mwananchi.


Jumla ya wateja wapya 40,000 wanatarajiwa kuunganishwa na huduma katika eneo la Salasala.

Mafundi wakiendelea kuchimba mifereji kwa ajili ya utandikaji mabomba ya maji katika mradi wa eneo la Salasala,utakaounganisha wateja wapya 40,000 baada ya mradi huo kukamilika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad