HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 29 September 2018

WANANCHI WALALAMIKIA WAFANYABIASHARA WALIOPANGA BIDHAA ZAO PEMBENI MWA BARABARA YA MWENDOKASI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Wananchi Mkoani Dar es  Salaam wanaotumia Barabara ya Msimbazi wamelalamikia wafanyabishara waliopanga bidhaa zao pembezoni mwa barabara ya mwendokasi.

Wafanyabiashara hao walioweka bidhaa zao pembezoni mwa barabara hiyo wamekuwa kero kubwa kwa wananchi hao kutokana na kukaa kwenye maeneo yanayopaswa kupita kwa miguu.

Wakitoa madukuduku yao, wananchi hao wamesema kuwa kwa sasa inawalazimu wapite kwenye barabara ya magari au mwendokasi badala ya kutumia maeneo waliyotengewa baada ya wafanyabiashara hao kuweka bidhaa chini.

Wamesema kuwa, kinachofanywa na wafanyabiashara hawa sio kitu cha haki na zaidi kinahatarisha usalama wao waenda kwa miguu kwani nara nyingi wamekuwa wanakoswa koswa na magari.

" kwanza wafanyabiashara hawa wamepanga bidhaa zao katika pande zote mbili, unakosa hata kwa kupita maana wamebana eneo lote inatulazimu kupita pembezoni mwa barabara ili kupita kwa urahisi ila napo pamekuwa na changamoto ya kunusurika kugongwa na magari na kuhatarisha maisha yetu," walisema.

Kika barabara hiyo ya Msimbazi, wafanyabiashara mbalimbali wameweka bidhaa zao pembezoni mwa njia ya wapita kwa miguu na imekuwa kero kubwa.

Ikumbukwe kuwa Wakati wa ufunguzi wa huduma ya mwendokasi, Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alitoa agizo la wafanyabishara wadogo wadogo wasipange bidhaa zao pembezoni mwa barabara ya mwendokasi, agizo ambalo lilifanyiwa kazi kwa kushirikiana na kampuni ya Strabag na Halmashauri kuajiri askari ambao walisimamia kikamilifu.

Aidha katika miezi ya karibuni  askari hao hawaonekani na kuwapa fursa wafanyabiashara hao kupanga bidhaa zao na kuleta usumbufu kwa wapita kwa miguu.
Wananchi wakipita katika barabara baada ya wafanyabiashara kupanga bidhaa zao kwenye njia ya wapita kwa miguu Kariakoo Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad