HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 19 September 2018

WAFANYAKAZI WA BENKI YA CRDB WAPATIWA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA MAJANGA YA MOTO

 Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Idara ya Udhibiti hali hatarishi, Anderson Mlabwa akizungumza jambo wakati wa kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa Benki hiyo juu ya kukabiliana na majanga ya moto pindi yanapotokea, yaliyoendeshwa na wakufunzi kutoka Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Makao Makuu, jijini Dar es salaam. Katikati ni Mkuu wa Chuo cha Zimamoto na Uokoaji nchini, Kamshna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto, Bakari Mrisho na kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB Kitengo cha Uendelezaji wa Biashara, Eng. Misana Mutani
 Mkuu wa Chuo cha Zimamoto na Uokoaji nchini, Kamshna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto, Bakari Mrisho akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa Benki hiyo juu ya kukabiliana na majanga ya moto pindi yanapotokea, yaliyoendeshwa na wakufunzi kutoka Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Makao Makuu, jijini Dar es salaam.
 Sehemu ya Wakurugenzi na Mameneja wa Benki ya CRDB wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Chuo cha Zimamoto na Uokoaji nchini, Kamshna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto, Bakari Mrisho (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao baada ya kumalizika kwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa Benki hiyo juu ya kukabiliana na majanga ya moto pindi yanapotokea, yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Benki hiyo, Mikocheni jijini Dar es salaam leo.
 Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Yusuph Nanyambo akitoa tathmini ya mafunzo hayo aliyowapatia wafanyakazi wa Benki ya CRDB.
 Sajenti Rajab Mwangalamo akitoa maelekezo ya namna ya kutumia kifaa maalumu cha muzimia moto kwenye magari madogo.

 Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Lumumba, Pendo Assey (kulia) pamoja na Meneje wa Benki ya CRDB Tawi la Viva Premier Club, Naomi Mwamfupe (kushoto) wakishirikiana kuzima moto wakati wa mafunzo ya vitendo ya uzimaji moto, yaliyokuwa yakitolewa na wakufunzi kutoka Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Makao Makuu, jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Kibaha, Rosemary Nchimbi akionyesha namna ya kuzima moto kwa kutumia kifaa maalum cha kuzimia moto kwa majumbani.
 Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen Killango akizima moto wakati wa mafunzo ya vitendo ya uzimaji moto, yaliyokuwa yakitolewa na wakufunzi kutoka Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Makao Makuu, jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad