HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 19 September 2018

KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUTAPERI KWA KUTUMIA JINA LA RAIS MSTAAFU

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu mkazi Kisutu imepanga Octoba 11, 2018 kuanza kusikiliza kesi ya kujitambulisha kwenye mitandao ya kijamii kwa kufungua vikoba vya kukopesha na kutumia jina la Rais mstaafu Jakaya Kikwete inayomkabili mtuhumiwa, Masse Uledi.

Masse anadaiwa kufungua akaunti ya vikoba kwa jina la Salma Kikwete vicoba Saccos na Ridhiwan Kikwete na kujifanya kuwa anakopesha hela kitendo kilichomwezesha kujipatia fedha kwa watu mbalimbali kwa njia ya udanganyifu.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita amedai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo ilikuja leo Septemba 19,2018 kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa Maelezo ya awali. (PH)

Akisomewa PH,, Mwita mbele ya Hakimu mkazi Mkuu, Thomas Simba, imedaiwa, Novemba 9, mwaka jana, mshtakiwa alijipatia sh. 840,000 kutoka kwa Joyce Chitumbi kiasi hicho kama dhamana ya kupata mkopo.

Pia mshitakiwa inadaiwa siku hiyo, alijipatia sh. 600,000 na sh. 200,000, kutoka kwa Daniel Cedalia ikiwa ni dhamana ya kupata mkopo wa sh. milioni mbili.

Katika shtaka la tatu imedaiwa, kati ya Septemba 28 na Oktoba mosi  mwaka jana  mshitakiwa alijipatia sh. milioni 2,160,000, kutoka kwa Lucas Kiula kama dhamana ya kupewa mkopo wa sh. milioni 10.

Pia  inadaiwa Novemba mwaka jana alijivika uhusika ambao sio wake kwa kutengeneza peji kwenye mitandao ya kijamii kwa kujitambulisha majina ambayo sio yake ambayo ni Jakaya Kikwete,Salma Kikwete, Getrude Rwakatale na Reginald Mengi kwa ajiri ya kujipatia fedha hizo.

Baada ya kusomewa maelezo hayo mshitakiwa amekiri taarifa zake binafsi ambazo ni jina lake, kufikishwa polisi na mahakamani huku akikana kuhusika na tuhuma hizo.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 11, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad