HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 19 September 2018

YANGA YAVUNA POINTI 3, MAKAMBO AFUNGA GOLI LA USHINDI

Na Agnes Francis, Globu ya Jamii.
Mabingwa wa kihistoria ligi kuu Tanzania Bara Yanga Sc wametoka kifua mbele kwa bao 1-0 dhidi ya wagosi wa kaya Coastal Union katika dimba la uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. 


Kipindi cha kwanza cha Mpira dakika 45 kilianza kwa kasi huku kila timu ikiitaji alama 3 kwa kulisakama lango la mwenzake. 

Katika kipindi cha kwanza dakika 11 mshambuliaji wa Yanga raia wa Kongo Heritie Makambo akaiandikia timu yake bao la kuongoza akipokea kwa pasi mujarabu iliyotolewa na Ibrahim Ajibu,na mpaka kipindi cha kwanza kimemalizika Coastal hawakupata goli.

Kipindi cha pili kilianza kwa kila upande kulisakama lango la mwenzake na kushambuliana kwa zamu huku Coastal Union wakilishambulia lango la Yanga kutafuta goli la kusawazisha,ambapo Yanga walionekana kuridhizika na matokeo hayo. 

Lakini Dakika za lala salama mchezo uligeuka kwa Yanga ambapo walionyesha kuamka kwa kuwashambia wapinzani wao kwa kulenga mashuti yasiokuwa na madhara kwa Coastal na mpaka Dakika 90 za mchezo matokeo ni 1-0. 

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema mazoezi ndio siri inayowafanya kushinda mechi zote mfululizo bila kupoteza mchezo hata mmoja. 

"Tatizo la wachezaji wangu wakishafunga goli huwa wanapotea mchezoni na hawafanyi vizuri kila mmoja anafanya anavyojua yeye"amesema kocha Zahera. 

Kocha wa Coastal Union Juma mgunda amezungumza na waandishi wa habari amesema kuwa watayafanyia kazi makosa waliyoyafanya mpaka kupelekea kikosi cha Yanga watumie nafasi hiyo kupata goli la kuongoza. 

Mgunda amelizungumzia swala la kuhusu kucheza kwa mchezaji wao Ali Kiba ambaye pia ni mwanamuziki wa bongo fleva hapa nchini kutokucheza tangu kuanza kwa ligi hiyo. 

"Ali ni mchezaji wetu Kama wechezaji wengine ikifikia muda wake nitamchezesha na kuitumikia timu yake". 

Yanga anaongoza ligi kuu Tanzania bara kwa alama 9 akiwa na magoli 7 ambapo amecheza michezo 3,atashuka tena dimbani septemba 23 kuwakaribisha Singida United uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Coastal Union kilichopambana na Yanga.

Kikosi cha Yanga kilichopambana na Coastal Union,
Kiungo wa Coastal Union Hassan Hamis akijaribu kumtoka Mshambuliaji wa Yanga Ibrahim Ajib wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliomalizika kwa Yanga kuondoka na ushindi wa goli 1-0 uliofanyika katika Uwanja wa Taifa. 
Kiungo wa Yanga Pappy Tshishimbi akimtoka beki wa Coastal Union Bakari Mwamnyeto wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliomalizika kwa Yanga kuondoka na ushindi wa goli 1-0 uliofanyika katika Uwanja wa Taifa. 
Mshambuliaji wa Yanga raia wa Kongo Heritie Makambo akishangilia goli baada ya kufunga dakika ya 11 wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliomalizika kwa Yanga kuondoka na ushindi wa goli 1-0 uliofanyika katika Uwanja wa Taifa. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad