HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, September 1, 2018

SERIKALI YAJIPANGA KUBHIBITI UCHELEWESHAJI WA KUPAKUA SHEHENA YA MAFUTA BANDARINI


 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaac Kamwele, kushoto akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya bandari na kituo cha kushushia mafuta cha KOJ.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaac Kamwele, wa pili kushoto akiangalia moja ya nondo zilizoshushwa bandarini kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya bandari na kituo cha kushushia mafuta cha KOJ. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko.  
 Mkandarasi wa mradi wa upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam (DMGP) kutoka Kampuni ya China Habour Engineering, LV Wei, kushoto akitoa maelezo ya mradi huo ulipofikia kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaac Kamwele, wa pili kulia na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya bandari na kituo cha kushushia mafuta cha KOJ.

SERIKALI yajipanga kubhibiti ucheleweshaji wa kupakua shehena ya mafuta bandarini
Dar es Salaam, Tanzania. Septemba 1, 2018. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema kwamba Serikali imejipanga kubhibiti ucheleweshaji wa kupakua shehena ya mafuta bandarini ili kubhibiti upandaji bei ya bidhaa hiyo kwenye soko la ndani.

Waziri Kamwelwe ameyasema hayo jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelea bandari ya Dar es Salaam katika eneo la Kurasini Oil Jet (KOJ), na kubaini kuwa wakati wa zoezi la upakuaji kunakuwa na tatizo la ucheleweshaji mbalo mwisho wa siku huchangia kuongezeka bei ya mafuta. 

Mh. Kamwele amesema kwamba wamegundua kuwa uwezo mdogo wa pampu za meli za kupakulia mafuta pamoja na uhaba wa matenki ya kuhifadhia mafuta kwa waagizaji wa bidhaa hiyo pamoja na kuvuja kwa mabomba ya mafuta ndio chanzo kikubwa cha kupanda bei.  

“Tumegundua kuwa tatizo lingine linalochangia kuongeza bei ya mafuta kuwa ni ucheleweshaji wa kupakua shehena hiyo ya mafuta kwani baadhi ya meli hazina pampu zenye wezo wa kusukuma bidhaa hiyo kwa nguvu inayotakiwa,” amesema waziri Kamwele.

Mhe Waziri amesema kwamba tatizo lingine alilogundua kuwa linachangia ucheleweshaji wa kupakua bidhaa hiyo sokoni ni waagizaji wa mafuta ambapo wengi wao huagiza shehena kubwa wakati uwezo wa matenki ya kuhifadhia mafuta hayo ni mdogo.

Mbaya zaidi amesema Waziri Kamwele kwamba gharama za ucheleweshaji huo kupelekwa kwa mtumiaji wa mwisho ambaye ni mwananchi. Kufuatia hali hiyo amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa TPA, kufanyia kazi suala hilo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko, amemuahidi Waziri kuwa atalisimamia hilo kikamilifu sababu ni kweli kwamba baadhi ya meli hazina pampu zenye nguvu ya kusukuma mafuta hayo kwa haraka.

Mhandisi Kakoko amesema kwamba kuhusu waagizaji mafuta atawasiliano nao tena kuwakumbusha juu ya hilo na kuwataka wawe wanaagiza mafuta kutokana na uwezo wao au waongeze idadi ya matenki ya kuhifadhia mafuta.

Ametolea mfano meli ambayo ilifunga mnamo tarehe 13/08/2018 na kukamilisha usukumaji wa mafuta kwa siku 11, jambo ambalo limesababisha ucheleweshaji mkubwa wa kupakua shehena hiyo kwa ajili ya soko.

“Makampuni yaliyokuwa yapokee mafuta siku hiyo yalikuwa ni zaidi ya 20 sasa ukichukulia meli kama hiyo ambayo ilikuwa ujazo wa mita karibu 104,000, ilitumia taribani siku 11 hali iliyosababisha wengine wachelewe kupata bidhaa hiyo sokoni,” amesema.

Ameyasihi maakapuni ya mafuta kuwa ni vyema yakaongeza matenki yao ya kuhifadhia mafuta au waagize kulingana na uwezo wao. Vinginevyo basi TPA haitolipa tozo zinazotokana na ucheleweshwaji huo bali kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe.

Meli ya mafuta ikikaa bandari kwa zaidi ya siku tano, TPA hulipa gharama za ukaji wa meli hiyo kwa kiasi cha US$ 25,000 kwa siku hadi meli hiyo itakapoondoka.

Kuhusu uvujaji wa mafuta, Waziri Kamwele ametoa maagizo kwa TPA kuwa wasipitishe tena mafuta kwenye mabomba au kwenye pacha za mabomba yanayovuja na kuongeza kuwa pia ni kinyume na utaratibu kupandisha bei ili kufidia hasara inayotokana na uvujaji huo.

Ameongeza kuwa kuendelea kupitisha mafuta kwenye mabomba yanayovuja kumefanya mwananchi ambaye ndio mtumiaji wa mwisho kubebeshwa mzigo usiostahili na kuongeza kwamba Serikali imeligundua hilo na kwa kuanzia itanunua ‘flow meter’ mpya na kuzifunga katika bandari zote. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko, amemuahidi Waziri huyo kuwa hawatoruhusu tena mafuta yaendelee kupita katika mabomba yanayovuja kwani kinachoonekana ni kuwa vifungashio vingine ambavyo vinatumika havikidhi matakwa ya kiubora katika kuhudumia bidhaa ya mafuta. 

“Kuna takribani makapuni 50 ya mafuta yanayopitisha bidhaa zao bandarini, tutawaandikia barua na kuwaelekeza waboreshe mabomba yao, kwa wale ambao watakaidi basi hatutapitisha mafuta yao kupitia miundombinu hiyo,” amesema Mhandisi Kakoko.

Katika hatua nyingine Mhandisi Kamwelwe alikagua mradi wa uboreshaji wa gati namba 1 hadi 7 katika bandari hiyo na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wake hadi sasa.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa TPA, ujenzi wa mradi huo unakwenda kwa kasi sababu unasimamiwa kwa ukaribu na watendaji wa TPA chini ya uongozi wake.

Amesema kwamba hadi sasa mradi huo umefikia asilimia 40 ya ujenzi wake ambapo upo mbele kwa asilimia 10 zaidi ya lengo lililopangwa.

Pindi mradi huo utakapokamilika utaifanya bandari ya Dar es Salaam kuwa ya kisasa zaidi na yenye uwezo mkubwa wa kuhudumia meli kubwa hadi za size ya Panamax ambazo ni moja ya meli kubwa na za kisasa zaidi duniani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad