HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 1 September 2018

MEYA WA DAR ES SALAAM AZIDUA MASHINDANO YA MASHAIRI

 Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akizungumza katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Mashairi ambayo yanaendelea katika ukumbi huo ambayo yameshirikisha washiriki 51 kutoka Dar es Salaam pekee.

Mkurugenzi wa Taasisi ya taaruma za Kiswahili wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Ernesta Mosha akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano ya ushairi yanayoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam leo Septemba 1,2018.
 Jaji wa mashindano ya mashairi, Nassoro Mhamed akizungumza na kuwapa moyo washiriki wa mashindano ya mashairi yanayofanyika jijini Dar es Salaam leo Septemba 1,2018.

Baadhi ya wahudhuriaji katika mashindano ya majaji.
 Wanafunzi wa shule za sekondari walikuja kuangalia mashindano ya mashairi yanayoendelea kufanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya washiriki wa mashindano ya mashairi.
Washiriki wa mashindano ya mashairi ambayo yanalengo la kukuza Lugha ya kiswahili nchini Tanzania.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

MEYA wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amezindua mashindano ya mashairi jijini Dar es Salaam leo yenye lengo la kukuza lugha ya kiswahili hapa nchini mashindano hayo yenye kauli mbiu  isemayo " Lugha yetu fahari yetu"

Mashindano hayo mgeni rasmi atakuwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ally Hasan Mwinyi washiriki wa mashindano hayo ni 51 ambapo mshindi wa kwanza atapata shilingi milioni moja, mshindi wa pili atapata shilingi lakitano, mshindi wa tatu atapata shilingi laki tatu na mshini wa nne mpaka kumi watapata shilingi laki moja moja.

Akizungumza katika uzinduzi huo wa mashairi ameomba lugha ya Kiswahili itumike barani Afrika kwa ujumla na Hapa nchini itumike kama Lugha ya kufundishia.

Amesema kuwa mashindano hayo hayataishia jijini Dar es Salaam tuu pia anategemea kuanzisha na mikoa mingine ya Tanzania. "Mashindano haya hayataishi jiji la Dar es Salaam tuu pia tutayaanzisha na mikoa mingine ya Tanzania"

Pia ameomba Lugha ya kiswahili iweze kurasimishwa katika nyanja za kisheria. kiafya pamoja kielemu kwa shule za msingi na sekondari pamoja na chuo kikuu ili mwanafunzi akifundishwa aelewe lugha na kitu anachofundishwa ili ajengewe uwepo wa kuelewa vizuri.

Nae Mkurugenzi wa Taasisi ya taaruma za Kiswahili wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dkt Ernesta Mosha amesema kuwa vitabu vya kufunsihia kidato cha kwanza mpaka cha nne vimeshatayarishwa kwaajili ya kufundishia ila bado havijalasimishwa tuu kutumika vitabu hivyo ni pamoja na Bayilojia, Hisabati, Jeografia na Historia ambavyo vimeandiskwa kwa lugha ya kiswahili fasaha bila kutohoa(translation)

Amesema kuwa tafiti zinaonesha kuwa kikwazo cha Istilahi sio tatizo kabisa kwa sababu mtu anajifunza kuanzia shule ha msingi mpaka chuo kikuu na lugha ya kiingereza iwe kama ya kujifunza ili kuwezesha mawasiliano ya kawaida.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad