HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 26 September 2018

RAIS ABBAS: JAPOKUWA SUALA LA PALESTINA LINAPITA KATIKA KIPINDI KIGUMU ZAIDI, LAKINI TUTASIMAMA KIDETE HADI KUFIKIA MALENGO YETU

Rais wa Dola ya Palestina Mheshimiwa Mahmuud Abbas, Jumanne ya tarehe 25/09/2018 akiwa mjini New York Marekani, amesema japokuwa suala la Palestina linapita katika kipindi kigumu zaidi, lakini taifa hilo la Palestina halitokata tamaa bali litaendelea kusimama kidete hadi kufikia malengo na maadili yetu ya kitaifa, ikiwa ni pamoja na kupata uhuru na kusimamisha dola yetu huru yenye mji mkuu wake Jerusalemu ya Mashariki.

Ameongeza kusema kuwa; hakika Utawala wa Marekani kwa maamuzi yake ya kuitambua Jerusalemu kuwa ni mji mkuu wa Israeli, kuhamishia Ubalozi wake mjini humo, kuondoa mafaili yanayohusu suala la wakimbizi kutoka katika meza ya majadiliano na kulikatia misaada shirika la UNRWA; Utawala huo wa Marekani utakuwa umejitoa wenyewe kutoka katika nafasi yake ya kuwa mpatanishi pekee wa mchakato wa kisiasa, vilevile kumekuwepo na ulazima wa kufanyika kwa mkutano wa amani wa kimataifa, utakaounda chombo cha kimataifa cha kusimamia mchakato huo wa amani.

Amesema hakika vitendo vya hatari vinavyofanywa na Israeli, ikiwemo kuendelea na sera yake ya kujenga makazi ya kilowezi na kuendeleza mashambulizi yake yanayolenga ardhi na watu wa Palestina haiwezekani kuyanyamazia, bali tutaendelea na jitihada zetu kwa ngazi zote, huku tukifikia maazimio mbalimbali kwa lengo la kulinda watu wetu na kuhifadhi haki zao zilizothibitishwa na sheria ya kimataifa.

Aidha Rais Abbas ameweka wazi kuwa, kuna vitisho vya wazi na vya hatari sana vinavyofanywa na Israeli, pale inapojaribu kudhoofisha nafasi na hali ya Msikiti Mtukufu wa Aqsa. Tunaionya Israeli juu ya maamuzi yake yoyote yanayolenga kujaribu kudhoofisha nafasi ya kidini ya Jerusalemu na Msikiti Mtukufu wa Aqsa, jambo ambalo litapelekea kuingia Ukanda wa Mashariki ya Kati katika mivutano zaidi na hali tete.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad