HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 20 September 2018

MWENGE WA UHURU KUTEMBELEA MIRADI 37 YA THAMANI YA SHILINGI BILIONI 15.7 MANYARA

MWENGE wa uhuru umepokelewa Mkoani Manyara ambapo utatembelea miradi 37 yenye thamani ya sh15.7 bilioni kwenye Halmashauri saba za mkoa huo. 

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti, akizungumza jana wakati wa kupokea mwenge huo kutoka Mkoani Arusha alisema utatembea miradi mbalimbali ya maendeleo, kwa kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi. 

Mnyeti alisema gharama ya miradi ya halmashauri ya wilaya ya Babati ni sh3.490 bilioni, Babati mji sh1. bilioni, Mbulu Mji sh1.1 bilioni, Halmashauri ya wilaya ya Mbulu sh3.4 bilioni, Hanang sh1.5 bilioni, Kiteto sh6.9 bilioni na Simanjiro sh1.1 bilioni.

"Tunawakaribisha kwenye mkoa wa Manyara ambapo wananchi wana hamu kubwa ya kuona mwenge wa uhuru na kusikiliza ujumbe wa elimu ni ufunguo wa maisha wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu," alisema Mnyeti. 

Mkuu wa Wilaya ya Babati Elizabeth Kitundu alisema kwenye halmashauri ya Wilaya hiyo mwenge wa uhuru utatembea miradi mitano ya thamani ya shilingi bilioni 3.4. 

Kitundu alisema mwenge wa uhuru utaweka jiwe la msingi kituo cha afya Nkaiti, bweni la wavulana shule ya msingi Mbugwe na kupanda miti ya kumbukumbu. 

Alisema utafungua daraja la Giheri kata ya Magara, uzinduzi wa kiwanda cha Hanang' Cotton Mill na uzinduzi wa mradi wa maji Gallapo. 

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Charles Kabeho aliwapongeza wananchi wa eneo hilo kwani kujitokeza kupokea mwenge huo. 

Kabeho alisema anatarajia kukuta miradi ya maendeleo yenye thamani ya fedha zitakazotajwa kwenye mkoa huo. 

Alisema hadi sasa mwenge wa uhuru umekimbizwa kwenye mikoa 29 yenye halmashauri 171 ikiwa bado halmashauri 25 na kuhitimisha mbio zake mkoani Tanga Octoba 13. 

Awali, Kaimu mkuu wa Mkoa wa Arusha, Idd Kimanta alisema mwenge wa uhuru ukiwa mkoani mwake umekimbizwa kwenye halmashauri saba za wilaya. 

Ukiwa Mkoani Manyara mwenge wa uhuru utakimbizwa kilomita 1, 575 kwenye wilaya za Babati, Mbulu, Hanang, Kiteto na Simanjiro. 
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti (kulia) akipokea mwenge wa uhuru kutoka kwa kaimu mkuu wa Mkoa wa Arusha, Idd Kimanta, ukiwa mkoani Manyara mwenge wa uhuru utatembelea miradi 37 yenye thamani ya shilingi bilioni 15.7.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akisoma taarifa ya mkoa huo baada ya kupokea mwenge wa uhuru kutoka Mkoani Arusha, ambapo utatembelea miradi 37 yenye thamani ya shilingi bilioni 15.7 kulia kwake ni kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Charles Kabeho.  
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa kwa mwaka 2018 Charles Kabeho akisoma jiwe la msingi la bweni la shule ya sekondari Mbugwe, Wilayani Babati, baada ya kuizindua, kulia ni Mkuu wa wilaya hiyo Elizabeth Kitundu. 
  Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Elizabeth Kitundu akipanda kwenye ukiwa katika halmashauri ya Wilaya ya hiyo mwenge wa uhuru umetembelea miradi mitano ya thamani ya shilingi bilioni 3.490.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti, akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Babati Elizabeth Kitundu mwenge wa uhuru baada ya kupokea kutoka Mkoani Arusha eneo la Minjingu madiwani. 

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad