HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 20 September 2018

Mawaziri watatu wakutana na jumuiya ya wafanyabiashara kujadili changamoto za biashara

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe akizungumza katika mkutano na Jumuiya ya wafanyabiashara kuhusiana na changamoto wanazokutana nazo katika biashara kupitia mamlaka za kiserikali.
  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango akizungumza na Jumuiya ya wafanyabiashara kwa kuwataka kufuata taratibu katika mamlaka zilizowekwa katika usimamiaji wa biashara hizo.
Waziri wa Viwanda biashara na uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza na jumuiya ya wafanyabiashara jijini Dar es Salaam leo.
Katibu wa Jumuiya ya wafanyabiashara  Abdallah Mwinyi akitoa hali mazingira ya biashara na changamoto wanzokutana nazo zinazotokana na mamlaka za serikali kushindwa kuweka usimamizi pamoja na sera na sharia.
 Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Charles Kichere akizungumza na Jumuiya ya Wafanyabiashara kuhusiana na ukusanyaji wa mapato na hatua ambazo wanazichukua kwa wafanyabiashara wasiofuata utaratibu.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko akizungumza kuhusiana na utaoji wa mizigo ya wafanayabiashara pamoja na hatua za ulipaji mapato ya serikali.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
JUMUIYA ya Waanyabiashara Kariakoo imekutana na mawaziri wa watatu kutoa changmoto zao biashara wanazokutana nazo na kufanya biashara zao kuwa ngumu.

Mwenyekiti wa Mkutano huo ambaye ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe amesema kuwa kukutana wa wafanyabiashara hao ni kutaka kujua changamto na kufanyia kazi ili serikali iendelee kupaata mapato.

Amesema kuwa maendeleo hayawezi kupatikana bila kuwepo kwa wafanyabiashara hivyo ni lazima kwa vongozi wenye dhamana kufanya kazi ya kukutana na wafanyabiashara kujua changamoto za biashara zinazotokana na mifumo ya kiutendaji serikalini.

Nae Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema kuwa wafanyabiashara wanahitajika sana katika maendeleo ya nchi kwani miradi inayotekezwa yanatokana na mapato ya ndani.

Amesema kuwa kuombaomba kunadharisha hivyo wafanyabiashara ndio nguzo ya maendeleo ikiwa ni kusoma bure kunatokana na hizo kodi ambazo ni za watanzania.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charle’s Mwijage amesema kuwa vitu vyote vilivyozuiliwa kwa ajili ya ukaguzi wa Shirika la Viwango Nchini (TBS) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kufanya ukaguzi bidhaa za wafabiashara kuanzi leo hadi kesho na kuma havikidhi mahitaji ya mlaji vitekezwe.

Hata hivyo Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere amesema kuwa kuna mchezo wa kwa wafanyabiashara wa Kariakoo kuchezea mashine za Kielektroniki ambapo wanashughulikia wote wanaofanya hivyo.


Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Mhandisi Deusdedit Kakoko amesema kuwa amepeleka maombi serikalini ya kuwepo kwa mkutano mara kwa mara kati ya wafanyabiashara na bandari ili kuweza kutoa huduma kwa wakati bila kufuata viongozi wajuu.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad