HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 28, 2018

MISA-TANZANIA YATOA TUZO YA UTOAJI WA TAARIFA KWA WIZARA, MASHIRIKA YA UMMA

Na Agness Francis, Globu ya jamii
TAASISI ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika (MISA) imetoa tuzo kwa mashirika mawili hapa nchini wakati wa kuadhimisha siku ya  kupata taarifa duniani kwa alieonesha ushirikiano wa kutoa taarifa na kwa aliebana  taarifa zake kwa umma mwaka 2018.

Ambapo tuzo ya ufunguo wa dhahabu ilikwenda Mfuko wa wahifadhi ya watumishi wa umma (PSPF) kwa kuonesha ushirikiano wa kutoa taarifa,ambapo zawadi ya kufuli la dhahabu imekwenda kwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kubana sana taarifa zao kwa mwaka huu.

Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam  Mjumbe wa MISA-Tanzania Rose Mwalimu
amesema tuzo hizo hutolewa Kila mwaka hapa nchini ambapo leo zimetoleo baada ya uzinduzi wa utafiti wa upatikanaji wa taarifa katika ofisi mbalimbali za umma.

Aidha Mwalimu amesema kwa mwaka huu utafiti huo umehusisha taasisi nane za umma kati ya hizo kuna Wizara nne, na taasisi ya wakala  wa Serikali nne.

Amezitaja  wizara hizo ni Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi,Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Wizara ya Viwanda na Uwekezaji.

Kwa upande wa taasisi ni Mfuko wa fedha kwa wafanyakazi (WCF),Mfuko wa Hifadhi wa Watumishi wa Umma (PSPF) ,Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB) na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

"Lengo la utafiti huu ni kuona jinsi gani wananchi wa kawaida wanapata taarifa zinazohusu maendeleo yao ama ya nchi  ili waweze kufanya maamuzi sahihi na kuchukua hatua stahiki kuhusu maisha yao binafsi na taarifa kwa ujumla"amesema Mwalimu.

Hata hivyo taasisi ya MISA Tanzania imetoa mapendekezo kuwa mafunzo yatolewe mara kwa mara kwa watumishi hasa kwa wale ambao wanatumika moja kwa moja na utoaji taarifa kwa umma  ili kujenga imani na wale wanaofika kwenye taasisi hizo kwa wenye nia ya kupata huduma mbali mbali,hasa mafisa habari,maofisa wa mapokezi na wale wa masjala.

Mwalimu amesema taasisi  hiyo ya MISA iliyoanzishwa 2002 Septemba 28 ikijumuisha nchi 11 za Kusini mwa Afrika (SADC) inayohusika na kufanya utafiti wa upatikanaji taarifa kwenye ofisi za  umma,ikiwa na lengo la kutetea na kuhakikisha uhuru wa habari na haki ya kupata taarifa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad