HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 27, 2018

MAHAFALI YA 18 YA TIOB YAFANYIKA DAR

Na Avila Kakingo,Globu ya jamii
TAASISI ya Taaluma za kibenki Tanzania(TIOB) imefanya mahafali ya 18 ambapo wahitimu 157 wametunukiwa vyeti

Sherehe za mahafali hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam ambapo pia wahitimu 22 wametunukiwa ngazi ya cheti, 133 wametunukiwa ngazi ya taaluma ya juu na 2 wametunukiwa vyeti vya kubobea katika masomo maalumu ya kibenki.

Pia katika sherehe za mahafali hayo wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika mitihani yao  walitunukiwa zawadi. 

Akizungumza wakati wa mahafali hayo  Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, .....  amesema  Sherehe ya mahafali zilitanguliwa na mkutano mkuu wa  20 wa mwaka kwaajili ya kutekeleza mpango wa 2018 wa TIOB pamoja na uteuzi wa Mkaguzi wa hesabu kwa mwaka 2018.

Aidha Amesema kuwa taasisi ya TIOB imetoa wahitimu  ambao wamebobea kwenye masuala ya benki. 

Pia amewashauri wahitimu wote kufanya kazi kwa weledi kutokana na mafunzo waliyoyapata pia amewapongeza wahitimu wote  kwa ushirikiano wao kwani wengine ni wafanyakazi wa taasisi mbalimbali za benki. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Benki TIOB Patrick Msusa amewapongeza Wahitimu wote .

Amewaomba watekeleze vyema majukumu yao katika kazi kwa misingi ya kibenki.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker, ambaye alikuwa mgeni rasmi akitoa hotuba yake.
 Picha ya pamoja.
 Mhitimu wa Taasisi ya Taaluma ya Kibenki Tanzania (TIOB), Emmanuel Mwakafwila, akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi wa Mafunzo TIOB, Marina Revelian, wakati wa mahafali ya 18 yaliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
 Mmoja wa wahitimu wa Mafunzo ya Ngazi ya Juu ya Kibenki, Givens Ernest, akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi wa Mafunzo TIOB, Marina Revelian, wakati wa mahafali ya 18 ya Taasisi ya Taaluma ya Kibenki Tanzania (TIOB)yaliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wahitimu wa Mafunzo ya Ngazi ya Juu ya Kibenki, Givens Ernest, akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi wa Mafunzo TIOB, Marina Revelian, wakati wa mahafali ya 18 yaliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Mhitimu wa Taasisi ya Taaluma ya Kibenki Tanzania (TIOB), Chibby Lusekelo Chibby, akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi wa Mafunzo TIOB, Marina Revelian, wakati wa mahafali ya 18 yaliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.  
 Maandamano yakianza.
Baadhi ya wahitimu.
 Wahitimu.
 Wahitimu.
 Wahitimu.
Wahitimu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker, ambaye alikuwa mgeni rasmi akitoa hotuba yake.
 Wahitimu.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TIOB, Patrick Msusa, akitoa hotuba yake katika mahafali hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad