HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 27 September 2018

CRDB Bank yazindua kampeni ya “Shinda na SimAccount”

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei (katikati) akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya utumiaji wa huduma ya kibenki kupitia simu ya mkononi ijulikanayo kama SimAccount katika promosheni ya “Shinda na SimAccount”, iliyofanyika jijini Dar es salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa CRDB Micro Finance, Sebastian Masaki pamoja na Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha nchini, Humud Mohamed.

Benki ya CRDB leo imezindua kampeni maalumu ya utumiaji wa huduma zake ya kibenki kupitia simu ya mkononi ijulikanayo kama SimAccount ambayo inawapa wateja wa benki pamoja na Watanzania kwa ujumla nafasi kujishindia fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 200.
Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo ijulikanayo kama “Shinda na SimAccount”, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei alisema Benki ya CRDB imeamua kuanzisha kampeni hiyo ili kuwahamasisha watanzania kujiunga na kutumia mfumo wa SimAccount ambao ni rahisi, nafuu na haraka.

Katika kampeni hii ya “Shinda na SimAccount”, wateja waliojiunga na kutumia huduma mbalimbali zinazopatikana ndani ya mfumo wa SimAccount watajishindia zawadi za fedha ambapo kila siku washindi 24 watakuwa wanapatikana, pamoja na washindi 12 wa wiki, washindi wa 3 wa mwezi na mshindi wa kampeni nzima "Jackpot Winner" atakaye patikana mwishoni mwa kampeni na kujishindia zawadi ya shilingi milioni ishirini.

"Unachotakiwa kufanya katika kampeni hii ni kujiunga na SimAccount kwa kupiga *150*62#, pamoja na kuitumia kufanya miamala mbalimbali ikiwemo kuweka na kutoa pesa kwenye matawi ya Benki ya CRDB, Mawakala wetu wa SimAccount na FahariHuduma Wakala” alifafanua Mkurugenzi huyo Mtendaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei (kushoto) akibonyeza kitufe kwenye luninga kuashiria uzinduzi wa kampeni maalumu ya utumiaji wa huduma ya kibenki kupitia simu ya mkononi ijulikanayo kama SimAccount iliyo chini ya Kampuni tanzu ya Benki (CRDB Micro Finance) katika promosheni ya “Shinda na SimAccount”, iliyofanyika jijini Dar es salaam leo. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Esther Mwambapa, Mkurugenzi wa CRDB MicroFinance, Sebastian Masaki pamoja na Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha nchini, Humud Mohamed. 

SimAccount ni mfumo maalum wa utoaji huduma unaowezesha watanzania kujisajili na kufungua akaunti kupitia simu za mkononi. Mfumo huu ulizinduliwa rasmi tarehe 26 Agosti Mwaka jana na Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano mama Samia Suluhu Hassan, ukiwa na lengo la kusaidia upatikanaji wa huduma za kifedha kwa urahisi na usalama kwa watanzania wengi hata wale wasio na akaunti za benki kupitia simu zao za mikononi “Simu Yako, Akaunti Yako”.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei (katikati) akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya utumiaji wa huduma ya kibenki kupitia simu ya mkononi ijulikanayo kama SimAccount katika promosheni ya “Shinda na SimAccount”, iliyofanyika jijini Dar es salaam leo.

Akielezea baadhi ya faida za kujiunga na mfumo wa SimAccount kwa wateja, Dkt Charles Kimei alisema mfumo huu unawapa fursa wateja;
  •  kufungua na kusimamia akaunti za vikundi mbalimbali ikiwemo vya kusaidiana, VICOBA, Harambee, harusi n.k.
  • uwezo kufungua akaunti mbalimbali kwa ajili ya kuweka akiba ili kutimiza malengo mbalimbali mteja aliyojiwekea.
  •  mfumo huu mteja ataweza kulipia manunuzi ya bidhaa kwenye maduka ya kawaida yanayopokea malipo kwa SimAccount kwa Mangi, Saluni, Mama Ntilie n.k
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei (kulia) akishuhudia zoezi la upigaji simu kwa washindo wa  promosheni ya “Shinda na SimAccount”.

Dkt. Kimei alisema uzinduzi wa kampeni hiyo ya “Shinda na SimAccount” unaleta chachu kwa watumiaji wa SimAccount kuendelea kufurahia huduma hizo huku wakijiweka katika nafasi nzuri ya kijishindia zawadi kubwa ya magari.

Akimalizia hotuba yake Dkt. Kimei alitoa rai kwa wateja na watanzania wote kwa ujumla kujiunga na SimAccount kwani ni mfumo madhubuti wa kibenki utakaowawezesha kufanya miamala yao kwa urahisi zaidi, pamoja na kijishindia zawadi mbalimbali katika kipindi cha miezi minne ya kampeni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad