HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 28 September 2018

INDONESIA YAAHIDI USHIRIKIANO NA TUME YA NGUVU ZA ATOMIKI TANZANIA

Na. VERO IGNATUS, ARUSHA.
Ubalozi wa Indonesia umeridhika na kazi zinazofanywa na Tume ya Nguvu za Atomiki Nchini katika kudhibiti matumizi ya nyuklia sanjari na kushirikiana katika kuhakikisha matumizi sahihi ya nyuklia yanakwenda katika sekta ya viwanda.
 
Akizungumza Balozi wa Indonesia Ratlan Pardede nchini Tanzania amesema upande kwa upande Indoneshia nyuklia wanaitumia katika viwanda na kilimo hivyo wanataka kuutumia uzoefu huo kwa kushirikiana na Tanzania ili kuinua uchumi kupitia teknolojia hiyo.

Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki nchini Profesa Lazaro Busagala amesema ujio wa Balozi wa Indonesia nchini a utaleta mafanikio katika sekta mbalimbali zinazotumia nguvu za nyuklia.

Profesa Busagala amesema mbali na kutembelea katika Kituo hicho cha Nyulkia kilichopo Jijini Arusha pia aliweza kutembembelea mahabara ya kuzalishia nguvu za nyuklia na amesema kituo hicho kipo katika hatua nzuri kwani kazi za ndani zimeshamalizika kwa sasa wanamalizia za nje.

Sambamba na hayo Balozi huyo amesema Mhe Rais Magufuli alimweleza Kwamba atafute maeneo mbalimbali nchini ambayo ataleta viwanda Tanzania kwa kupitia wafanyabiashara mbalimbali na ndicho anachochokifanya kwa sasa.

Uwezekano wa Indonesia kuleta viwanda vinavyotumia teknlojia ya nyuklia na madawa, uchumi wa Tanzania utaongezeka kwani unaendana na sera sahihi ya serikali wa kujenga Tanzania ya viwanda.

'' Tunapoongelea teknolojia ya nyuklia tunaongelea uwezekano wa kiwa na viwanda vingi zaidi uchumi wa nchi utaongezeka. "alisema Busagala.

Licha ya nchi ya Indonesia kufanya vizuri katika viwanda, huku Tanzania nayo ikiweka mkazo na msisitizo katika uongezaji wa viwanja ameeleza ushirikiano huo wa Teknolojia mpya utasaidia nchi ya Tanzania kuondokana na upotevu wa asilimia 40 ya mazao ya kilimo na kuongeza mapato ya nchi kwa kiasi kikubwa
Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Profesa Rtlan Pardede akizungumza na menejimenti ya Nguvu ya Atomiki iliyopo Njiro Jijini Arusha. Picha na Vero Ignatus
 Mkurugenzi mkuu wa Nguvu za Atomiki nchini Profesa Lazaro Busagala akizungumza mara baada ya kuwasili ugeni kutoka Ubalozi wa Indonesia katika Makao makuu ya Ofisi hiyo iliyopo Njiro Jijini Arusha. Picha na Vero Ignatus.
Kaimu Mkurugenzi - Kurugenzi ya matumizi ya Teknolojia ya Mionzi Yesaya Sungita akimuonyesha Balozi wa Indonesia mahali pa kufanya vipimo na kuangalia usalama wa vyakula, Mahali pa kufanyia utafiti wa vitu vinavyotoa mionzi.
Mkuu wa Idara ya Mionzi  DennisMwalongo (watatu kulia) akitoa maelekezo kwa Balozi wa Indonesia Profesa Ratlan Pardede namna ambavyo mashine za kuhakiki, vifaavya mionzi, mashine za Kupima mionzi katika mwili wa Binadamu kama kuna dharura au ajali, wa pili kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Nguvu ya Atomiki Nchini Profesa Lazaro Busagala. Picha na Vero Ignatus. 
Mgeni rasmi Balozi Indonesia Nchini Profesa Ratlan Pardede, akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya nguvu za Atomiki Nchini Profesa Lazaro Busagala, aliyepo kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Fedha  Aquline Kessy, Mkurugenzi wa kinga ya mionzi John Ben Ngatunga na Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya matumizi ya Teknolojia ya Mionzi Yesaye Sungita. Picha na Vero Ignatus
Picha ya pamoja na Mgeni rasmi Menejimenti ya Tume ya Nguvu ya Atomoki na baadhi ya viongozi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Picha na Vero Ignatus.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad