HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 28 September 2018

Arusha United Wanautalii kuivaa Rhino Rangers Septemba 29/2018

 Kikosi cha timu ya Arusha United  wanautalii kama wanavyoonekana pichani. 
Msemaji wa timu ya Arusha United wana utalii Jamillah Omar

Na. VERO IGNATUS, ARUSHA
Ni septemba 29/2018 ni siku ua  kuanza rasmi ligi daraja la kwanza msimu wa kwanza  wakazi wa jiji la Arusha na viunga vyake wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu ya Mkoa huo ya Arusha United Wanautalii siku ya tarehe 29 wakati timu hiyo itakapomenyana na Rhino Rangers Fc ya Tabora.

Msemaji wa timu ya Arusha United wana utalii Jamillah Omar akizungumza na waandishi wa habari  katika uwanja wa Shekh Amri Abeid  amesema anatarajia wana Arusha watajitokeza kwa wingi siku hiyo ili kuishangilia timu hiyo ambayo kwa sasa inarudisha Mkoa huo  katika ramani ya soka nchini ambayo imepotea kwa muda mrefu.

Jamillah amesema kikosi cha timu ya Arusha United  wanautalii kimedhamiria  kuingia ligi kuu mwakani kutokana na kuwa na kikosi imara chini ya kocha mkuu Felix Minziro  ambae anahistoria safi katika soka nchini.

Kaimu Mkurugenzi mtendaji  wa timu ya Arusha United wana utalii Fikiri Elias amesema timu yake imejiandaa vyema kukabiliana na timu ya Rhino Rangers Fc kutoka Tabora na wauhakika na ushindi wa point tatu.

Kwa mara ya kwanza tangu ipate usajili timu ya Arusha United wana utalii itajitupa uwanjani rasmi kuanza kushiriki ligi daraja la kwanza mwaka huu ikiwa katika safari yake ya kuelekea ligi kuu mwakani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad