HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 16 September 2018

DAWASA WAANZA KUDHIBITI UVUJAJI WA MAJI TABATA

* Yazindua siku tatu za kumaliza tatizo la uvujaji maji katika kata 11.Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) wamezindua uzibaji wa mivujo ya mabomba inayomwaga maji katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani wakianzia katika maeneo ya Tabata zoezi litakalodumu kwa muda wa siku tatu ikiwa ni katika kutekeleza miradi mbalimbali ndani ya siku 100.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji Mhaandisi Aron Joseph alipozindua mkakati huo wa kuhakikisha maeneo yote yanayotiririsha maji kutoka kwenye miundo mbinu ya Dawasa yanafanyiwa kazi kwa asilimia 90 na kisha kukabidhi kwa Meneja wa Dawasa Mkoa wa Tabata.

Akielezea zoezi hilo lilioanza leo, Aron amesema kuwa watatembelea maeneo yote ya Tabata yenye kata 11 zinazopata huduma za maji na kupambana na mivujo na tayari wataalamu wameshaingia kazini kwa ajili ya kuyafanyia kazi.

"Kuna timu zaidi ya watu 70 katika maeneo 20 tofauti ndani ya Tabata ambapo kuna kata 11 yenye maji na watalaamu hao wote wapo kuhakikisha mivujo yote inayojulikana na ile mipya wanafanyia marekebisho maeneo hayo yamefanyiwa kazi ndani ya siku tatu na iwe imeondoka,"amesema Aron.

Amesema nia na madhumuni ya kufanya zoezi hili ni kuhakikisha eneo lote la Tabata lenye maeneo sugu na mapya yanayovuja kupatiwa ufumbuzi na iwe imeondoka kabisa na katika hilo na wamemtaka Meneja wa Dawasa Mkoa wa Tabata kuhakikisha inapotokea mivujo anatakiwa kuidhibiti na kuziba ndani ya masaa 6.

Aron amesema kuwa anatambua kuna baadhi ya maeneo ya Tabata na sehemu zingine miundo mbinu yake ni chakavu na hilo suala linajulikana, kama Dawasa mpya wameweka mikakati ya kuhakikisha ndani ya miaka mitatu miundo mbinu hiyo inabadilishwa na ili wananchi wasikose maji idara ya uzalishaji na usambazaji maji utahakikisha katika kipindi chote hicho watakuwa wanasimamia miundo mbinu hiyo ili kuondokana na uvujaji wa maji.

Akiongezea, Aron amewasihi wananchi kutoa taarifa kwa Mamlaka husika pindi wanapoona maji yanavuja kupitia namba yao ambayo haina malipo pia hata watakapowaona mafundi wa Dawasa wawape taarifa ili wakarekebishe eneo hilo.

Meneja wa Usambazaji maji Mhandisi Paschael Fumbuka amesema zoezi hili ni kwa ajili ya kuhakikisha wanaboresha miundo mbinu ya maji kwa kuzuia upotevu wa maji kitu ambacho kinaathiri biashara ya maji maana kila tone la maji linahesabiwa.

Fumbuka ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na Dawasa kuwabaini watu wanaochafua miundo mbinu yao ikiwamo kutiririsha maji taka na hatua za kisheria zitachukuliwa juu yao.


Dawasa wameanza kutekeleza moja ya mikakati yao siku 100 ya kumaliza miradi mbalimbali na changamoto ikiwemo uvujaji wa maji kutoka katika miundo mbinu yao.
 Baadhi ya mafundi waliokatika maeneo mbalimbali ya Tabata wakiziba uvujaji wa maji baada ya kuzinduliwa na  Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Mkoa wa Dar  es Salaam (DAWASA) utakaofanyika kwa muda wa siku tatu.

Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji  wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Mkoa wa Dar  es Salaam (DAWASA) Mhandisi Aron Joseph akizungumza na waandishi wa habari waliofika katika baadhi ya maeneo yanayofanyiwa ukarabati wa uzibaji wa mabomba uliozinduliwa na utachukua siku tatu kukamilisha eneo la Tabata.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad