HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 26 September 2018

Chuo Kikuu mzumbe chaendesha Mafunzo ya Usafrishaji na Manunuzi


 Mratibu wa mradi huo katika Chuo Kikuu Mzumbe Dk. Omary Swalehe akizungumza na waandishi habari kuhusiana na mradi wa masuala ya usafirishaji na manunuzi.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
CHUO Kikuu Mzumbe kimesema kinaendelea kutoa elimu bora ikiwa ni katika kuendana na wakati ya kuhakikisha taaluma inayotolewa ni endelevu.

Hayo ameyasema Mkuu wa Tawi la Dar es Salaam Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Honest Ngowi wakati akifungua mafunzo ya masuala ya usafrishaji na manunuzi kwa taasisi mbalimbali za ulinzi, mamlaka na Halmashauri katika kuhakikisha masuala ya usafirishaji na manunuzi yanaleta maendeleo.

Amesema mafunzo hayo yanafadhiliwa Taasisi ya Kuehne na kuendeshwa na  Chuo Kikuu Mzumbe amesema kuwa aliyeanzishwa taasisi hiyo amekuwa bilionea katika masuala ya usafirishaji na manunuzi ambapo ni kuhakikisha watu wanapata mbinu mpya za usafirishaji na manunuzi.

Mratibu wa mradi huo katika Chuo Kikuu Mzumbe Dk. Omary Swalehe amesema kuwa mradi huo ni wa miaka mitatu ambapo nia kutoa mafunzo kwa taasisi mbalimbali katika masuala ya usafirishaji na manunuzi.

Amesema kuwa hadi sasa wameshafanya katika awamu mbili ambapo katika maeneo tofauti ikiwa ni kuwajengea mbinu mpya za usafrishaji na manunuzi na kuweza kuona tija katika maendeleo ya nchi.
 Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Tawi la Dar es Salaam Profesa Honest Ngowi akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo ya watu wa masuala ya usafirishaji na manunuzi wa taasisi za Serikali na Ulinzi katika Tawi hilo.
Baadhi ya wadau wakiwa katika mafunzo ya usafirishaji na manunuzi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad