HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 26 September 2018

JONESIA RUKYAA AKABIDHIWA RUNGU DERBY YA SIMBA NA YANGA

Na Agness Francis, Globu ya jamii.
ZIKIWA zimesalia Siku nne kuelekea mpambano wa  watani wa jadi Simba na Yanga kufanyika   katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar as Salaam, Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) limemtangaza mwamuzi wa kati atakayecheza mechi hiyo.

Mchezo huo  wa Ligi kuu wa Tanzania Bara (TPL) utachezwa  Septemba 30 siku ukiwakutanisha miamba ya soka Nchini Simba na Yanga kuanzia majira ya saa 11 jioni.

Akizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam, Afisa Habari wa TFF, Cliford Ndimbo amesema kuwa mcezo huo utakaoanza saa 11 jioni utachezeshwa na Mwamuzi kutoka Mkoani Kagera Jonesia Rukyaa mwenye eji ya FIFA akisaidiwa na waamuzi wa pembeni Ferdinand Chacha wa Mwanza na Mohamed Mkono kutoka Tanga. huku msaidizi wa mezani akiwa Heri Sasii.

Amesema kuwa, mbali na michezo hiyo kutakuwa na mechi zingine za ligi kuu zitakazoendelea kwenye viwanja tofauti kuanzia kesho Alhamisi mpaka Jumamosi kukamilisha mzunguko wa nane na wa tisa.

Katika kuelekea mchezo huo wa vuta nikuvute kikosi cha Simba  kilichoweka  kambi yake   Jijini Dar es Salaam kitamkosa mshambuliaji wake mahiri John Boko aliyepewa kadi nyekundu  katika mchezo uliopita na mwadui fc,Apambo Yanga wakiwa mji kasoro bahari Morogoro kwa matayarisho ya mtanange huo.

Michezo iliyopita simba walitoka na ushindi wa mabao 3-1dhidi ya wachimba Madini  Mwadui ya Shinyanga, Yanga wakiibuka  kidedea kwa kuwafunga walima alizeti  Singida United mabao 2-0.

Kurwa na Doto hao wametofautiana pointi mbili ambapo Yanga ana alama 12 wakiwa wamecheza michezo 4,huku wekundu wa msimbazi Simba wana pointi 10 michezo 5 ligi kuu Tanzania bara TPL.

Timu hizo zimekutana kwa mara ya mwisho ligi kuu ya msimu wa 2017/18 Simba wakitoka na ushindi wa goli 1-0 goli likifungwa na Erasto Nyoni.

Jonesia aliwachezesha Simba na Yanga katika msimu wa 2016/17 Yanga akiibuka kidedea kwa kuondoka na ushindi wa goli 2-0.

Mashabiki wa pande zote mbili wakiwa na shauku kubwa  ya siku hiyo kushuhudia mchezo huo utakopigwa  jumapili hii septemba 30 majira ya saa 11 jioni kujua nani mbabe kati ya majirani hao wa Kariakoo kwa kiingilio cha VIP A  30000,VIP B na C 20000,kwa viti vya bluu,kijani na rangi ya chungwa ni 7000.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad