HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 2 August 2018

WAZIRI WA ELIMU ATEMBELEA MAONESHO YA WANASAYANSI CHIPUKIZI

 Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Joyce Ndalichako ametembelea maonesho yanayofanywa na wanafunzi kutoka shule za Sekondari nchini zikiwa zimelenga gunduzi za kisayansi kwa wanajamii.

Akizungumza na vyombo vya habari Ndalichako ameeleza kufurahishwa na vijana hao kwa ubunifu na gunduzi walizozifanya.

Aidha ameitaka mmlaka ya sayansi na teknolojia nchini (COSTECH) kuwatazama kwa jicho la tatu wanafunzi hao waliofanya maonesho hayo.

Kuhusu shule za vipaji na kuziendeleza Ndalichako amesema kuwa kuna utaratibu wa kurudisha kasi ya shule hizo ziwe kama zamani kwa kuwa kuna ulegevu katika usimamizi.

Pia ameeleza kuwa lazima serikali iwe na shule ambazo ni chachu katika kuzalisha wataalamu na amefurahi kuwa shule zilizoongoza katika matokeo ya kidato cha sita ni pamoja na zile za serikali.

Ndalichako amewataka wanafunzi wengi zaidi kujitokeza kuonesha ubunifu wa kisayansi katika kutatua matatizo katika jamii.

Maonesho hayo yaliyoandaliwa na taasisi ya Young Scientist (YS) na kushirikisha shule za Sekondari Tanzania bara na visiwani.

Mwisho.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Joyce Ndalichako akiwakabidhi  zawadi   washindi wa YST 2018 wanafunzi wa kidato cha nne katika  shule ya wasichana ya Msalato iliyopo jijini  Dodoma,Farida  Mnyazi na Wilhelmina Martin jana jijini Dar as Salaam.
 Waziri wa Elimu na Mafunzo yab Ufundi Joyce Ndalichako akiwa katika banda la shule ya sekondari Vingunguti akipata maelezo mafupi kutoka kwa  Neema julius (kulia) alipotembelea banda lao katika maonesho ya sayansi na teknolojia leo jiji Dar as Salaam.(Picha na Emmaniel Massaka Globu ya jamii)

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya elimu Joyce Ndalichako akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua maonesho hayo.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad