HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, August 18, 2018

Ujenzi wa Daraja la Ikungulyabashashi kuhimarisha Mawasiliano ya Usafirishaji Simiyu

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akifungua Daraja la Ikungulyabashashi wilayani Bariadi mkoani Simiyu, wakati Mwenge wa Uhuru ukiwa katika mbio zake wilayani humo, Agosti 17, 2018.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Daraja la Ikungulyabashashi wilayani Bariadi mkoani Simiyu, wakati Mwenge wa Uhuru ukiwa katika mbio zake wilayani humo, Agosti 17, 2018.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akizungumza na Wanafunzi wanachama wa Klabu ya Wapinga Rushwa katika Shule ya Sekodari Nyasosi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, wakati Mwenge wa Uhuru ukiwa katika mbio zake wilayani humo, Agosti 17, 2018.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akiangalia kiatu kilichotengenezwa na Kikundi cha Vijana wa Dutwa wilayani Bariadi Mkoani Simiyu, wakati Mwenge wa Uhuru ukiwa katika mbio zake wilayani humo, Agosti 17, 2018.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho akimtwisha ndoo ya maji Bi. Joyce Paulo mkazi wa Kijiji cha Kasoli wiayani Bariadi mkoani Simiyu mara baada ya kufungua mradi wa kisima kirefu cha maji Kasoli, wakati Mwenge wa Uhuru ukiwa katika mbio zake wilayani humo, Agosti 17, 2018.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho na viongozi wengine w Wilaya ya Bariadi wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Festo Kiswaga(kulia) wakishangilia mara baada ya kiongozi huyo kufungua Shule ya Otto Busese (iliyojengwa kwa ufadhili wa Alliance Ginnery Limited), wakati Mwenge wa Uhuru ukiwa katika mbio zake wilayani humo, Agosti 17, 2018.
Mkimbiza Mwenge Kitaifa mwaka 2018, Ndg Ipyana Alinuswe Mlilo akitoa Ujumbe wa Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 katika Shule ya Sekondari Kasoli wiayani Bariadi, wakati Mwenge wa Uhuru ukiwa katika mbio zake wilayani humo, Agosti 17, 2018.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhandisi. Wilbert Siogopi akimkaribisha Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho, kabla ya kukabidhiwa Mwnge wa Uhuru na Mkurugnezi mwenzake wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi , Ndg. Melkizedeck Humbe Agosti 17, 2018.

Na Stella Kalinga, Simiyu

Wananchi wa Vijiji vya Mkuyuni, Ikungulyabashashi, Mwahalaja na Lulayu Kata ya Ikungulyabashashi, wilayani Bariadi Mkoani Simiyu wameishukuru Serikali kwa kukamilisha ujenzi wa Daraja la Ikungulyabashashi na kukiri kuwa kukamilika kwa daraja hilo kutarahisisha na kuimarisha mawasiliano na usafirishaji.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya wananchi kutoka katika kata Vijiji hivyo mara baada ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho kufungua daraja hilo, wakati Mwenge wa Uhuru ukiwa katika mbio zake wilayani Bariadi Agosti 17, 2018.

Wamesema awali kabla ya kukamilika  kwa daraja hilo walikuwa wakipata changamoto ya kusafirisha mazao na mifugo yao  na wakati mwingine kusafiri wao wenyewe hususani kipindi cha masika hivyo kufanya mawasiliano kuwa magumu kati ya pande mbili zinazotenganishwa na daraja hili.

“Kukamilika kwa daraja hili kutaongeza uzalishaji kwa kuwa mawasiliano ya pande zote mbili yatakuwa vizuri tofauti na mwanzo ambapo tulikuwa tunapata shida ya kusafirisha mazao yetu, mifugo  na sisi wenyewe kusafiri kutoka upande mmoja hadi mwingine hasa wakati wa masika” alisema Joshua Yakobo mkazi wa Kilalo.

 “Tunaishukuru sana Serikali kukamilisha Daraja hili ambalo litarahisisha sana mawasiliano sasa hivi wakazi wa vijiji vya Kata ya Ikunguyabashashi watakuwa wanavuka katika daraja hilo kwenda kufanya biashara katika minada ya Dutwa, Nyakabindi na Bariadi Mjini” alisema Benjamin Malala.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018, Ndg. Charles Kabeho alikagua ujenzi wa daraja hilo na kuridhishwa hatimaye akaupongeza Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi kwa kujenga daraja hilo kwa kuzingatia viwango.

Akisoma taarifa ya Ujenzi wa Daraja hilo Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini naVijijini(TARURA), Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhandisi. Nyamagalula Masatu amesema daraja la Ikungulyabashashi lenye urefu wa mita 16.8, upana wa mita 6.6 linajengwa kwa ufadhili wa Department For International Developments (DFID) kwa usimamizi wa TARURA.

Ameongeza kuwa ujenzi wa daraja hili utagharimu jumla ya shilingi 345,293,434/= huku akibainisha kuwa faida kuu ya mradi huu ni kurahisisha usafirishaji wa mazao ya kilimo kutoka mashambani kwa wakulima kwenda kwenye masoko.

Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi umepita katika miradi minne yenye thamani ya shilingi milioni 568 ikiwemo mradi wa maji wa Kasoli na Shule ya Msingi Otto Busese ambayo imejengwa kwa ufadhili wa Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginnery Limited kiilichopo Kasoli Bariadi.

Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Kuchambua Pamba cha Aliance Ginnery, Bw. Boaz Ogola amesema kuwa Kampuni yake inatambua kuwa nayo ni sehemu ya jamii, hivyo imeamua kushirikiana na jamii katika kuchangia maendeleo ya huduma za jamii katika elimu, afya na maji.

“Tumeshirikiana na jamii katika kuimarisha huduma za jamii,  Kasoli tumechimba kisima cha maji, tumejenga madarasa mawili na matundu matano ya vyoo katika kila shule inayotuzunguka, tumejenga Bweni la watoto wa kike katika shule ya Sekondari Mwamlapa na tunaendelea kushirikiana na jamii kuhakikisha kuwa tunaunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha elimu” amesema Ogola.

Mwenge wa Uhuru unaendelea na mbio zake mkoani Simiyu ambapo Agosti 18 utakuwa katika Wilaya ya Busega, Agosti 19 utakuwa katika Wilaya ya Maswa na Agosti 20 utakabidhiwa katika Mkoa wa Shinyanga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad