HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, August 18, 2018

GULAMALI AMUOMBA WAZIRI MKUU KUONDOA FAINI KANDAMIZI KWA WAKULIMA WA PAMBA WILAYANI IGUNGA

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii.
MBUNGE wa Jimbo la Manonga  Mh. Seif Khamis Gulamali amemuomba Waziri Mkuu  Mh. Kassim Majaliwa kutoa tamko juu ya faini zinazotozwa kwa wakulima wa Pamba Wilayani Igunga wakati huu wa urejeshaji wa mbegu za Pamba.

Akieleza hayo kwa Waziri Mkuu aliyeko ziarani Mkoani humo Gulamali amesema kuwa faini hizo zilikuwa zinalipishwa bila hata risiti na baada ya kumuomba Mkuu wa Mkoa alitekeleza kwa kuagiza ofisi ya Mkuu wa Wilaya (Igunga) kutotoa risiti kwa faini zozote.

Gulamali ameeleza kuwa faini hizo  zimekuwa kero kubwa kwa wakulima wa Jimbo lake la Manonga na kwa masikitiko makubwa amesema zinatekelezwa Igunga tu lakini hazipo kabisa Wilaya ya Nzega ambapo kilimo cha pamba kinafanyika pia.

Aidha Alimwomba Waziri Mkuu kutoa tamko juu ya faini hizo zinazowanyanyasa wakulima ndani ya Wilaya ya Igunga hasa katika Jimbo la Manonga. Pia Gulamali alihoji  zinapokwenda fedha hizo za faini kwani mpaka sasa haieleweki.

Akijibu kero hiyo, Waziri Mkuu ameonesha kuchukizwa na faini hizo na amemuagiza Mkuu wa Wilaya apitie upya Sheria hiyo na Madiwani kwani haimpendezi hata kidogo.

 Akihutubia mamia ya wakazi wa Jimbo la Bukene, ameeleza kuwa faini hiyo kwenye Pamba inakosa maana kwani msimu haujafika mwisho na amempongeza Mh. Gulamali kuwatetea wapiga kura wake.

 Waziri Mkuu amemtaka Mkuu wa Wilaya Kukaa na Madiwani wa Halmashauri na Wampe Taarifa Mh. Gulamali kwa kuwa wakati Mwingine vikao huitishwa na Mbunge hapewi Taarifa na Amemuomba Mh Mbunge kuendelea na ari hiyo hasa kwenye vikao vya baraza la Madiwani ambavyo yeye ni mjumbe pia.
 Mbunge wa Manonga Seif Gulamali akizungumza katika ziara iliyofanywa na  Waziri mkuu Kassimu Majaliwa Mkoani Tabora.
Wakazi wa Jimbo la  Bukene waliojitokeza kumsikiliza Waziri Mkuu katika ziara yake Mkoani Tabora.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad