HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 2 August 2018

TULIA TRUST YAWAPELEKA WATOTO WATANO KUSOMA NCHINI NIGERIA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Taasisi ya Tulia Trust  inayojihusisha  na masuala ya Afya na Elimu nchini imeweza  kuwasaidia watoto mbalimbali  wanaoishi katika mazingira magumu na wengine kutoa fursa kwa vijana watano (5) kwenda kuendelea  na elimu yao ya Sekondari Nchini Nigeria.

Tulia Trust ni shirika  lisilo la kiserikali Trust  lilianzishwa mwaka 2015 na  Mheshimiwa. Dk. Tulia Ackson, Naibu Spika wa Bunge la  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Balozi wa Tulia Trust Dotto Bernad Bwakeya ' Lameck Ditto" amesema kuwa katika  kuchangia  na kusaidia  sekta ya Elimu Tulia Trust imetoa  nafasi ya pekee kwa vijana watano (5) ambao watakwenda  kuendelea na masomo ya sekondari Nchini Nigeria katika Taasisi ya  Rochas Foundation College of Africa.

Ditto amesema Kupitia  ziara mbalimbali  za Dkt. Tulia katika Shule za Sekondari mkoani  Mbeya alifanikiwa kukutana na  kuunganishwa na  vijana hao  ambao wengi wao wanatoka katika hali  duni kiuchumi, yatima na wengi wao wanalelewa na mzazi  mmoja au ndugu. 

Amesema jitihada zilizofanywa na Tulia Trust ni kuhakikisha vijana hawa ambao kielimu wamekua wakifanya  vizuri achilia mbali changamoto walizonazo kiuchumi na waliweza kufaulu vizuri mitihani ya darasa la saba ni kuwapatia msaada wa kielimu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Taasisi ya Rocha Foundation imekuwa inashirikiana na taasisi mbalimbi barani Afrika ili kuwawezesha watoto wanaoishi katika mazingira magumu kupata  nafasi ya kujiendeleza kielimu na tayari watoto wengine watano kutoka Dar es Salaam wameshapatikana nao wataelekea nchini Nigeria.

Nchini  Nigeria Vijana  hao Wataendelea na  masomo mpaka kumaliza  Elimu ya Sekondari, Tulia Trust itakua nao bega  kwa bega mpaka wanahitimu Elimu zao za Sekondari , hii ni katika  kuhakikisha wanapata Elimu bora.

Moja  ya watoto hao Anne Bernad  Shitindi ameishukuru  Taasisi ya Tulia Trust kwa kuwapatia nafasi ya kwenda kujiendeleza  kielimu nchini Nigeria na akiahidi kufanya vizuri katika masomo yako na kupeperusha vyema bendera  ya Tanzania.

Mzee Lupyuto Mwamakula Ngubi ambaye ni Mlezi wa Mtoto Anna Bernad amewashukuru Tulia Trust  kwa ufadhili huo wa Elimu  kwa kijana wake ambaye alipoteza wazazi wake wote wawili akiwa  bado mdogo. Amesema fursa hii itamsaidia Anna kupata Elimu nzuri na amemtaka yeye pamoja na wenzake  wakasome kwa bidii.

Tulia Trusy imetoa nafasi hiyo kwa watoto wa kike wanne na wakiume mmoja ambapo Majina ya watoto ni hayo ni Anna Bernad Shitindi, Ayubu Andrea Mwaihola, Suzana Willy Mwakilima, Bernada Emmanuel Fuime, Beautiful Japhary Msinge na wataondoka alfajiri ya Ijumaa ya Agost 03 mwaka huu.
 Balozi wa taasisi ya Tulia Trust, Dotto Bernad 'Ditto' akDitto'mza  na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar as Salaam, juu ya Taasisi ya Tulia Trust inavyolenga katika kuwasaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na kutoa fursa kwa vijana watano  kwenda kusoma elimu ya  sekondari nchi ya Nigeria.(Picha zote na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
 Mlezi wa mtoto Anna Bernad, Mzee Lupyuto Mwamakula akizungumza na waandishi wa habari  leo jijini Dar as Salaam,ambapo ameishukuru Taasisi ya Tulia Trust kwa kumpeleka kijana wake  kusoma nchi Nigeria.
Picha ya pamoja

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad