HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 16, 2018

TAARIFA KWA UMMA: KUANZA KWA MFUKO PSSSF NA HUDUMA ZA MIFUKO YA PENSHENI ILIYOUNGANISHWA

Mnamo Tarehe 1 Agosti, 2018 Sheria Na. 2 ya 2018 inayounda Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ilianza rasmi kutumika kwa mujibu wa Tangazo la Serikali Na. 375 la Tarehe 27 Julai, 2018. Sheria hii pamoja na mambo mengine inaunganisha Mifuko ya Pensheni minne (4) ambayo ni Mfuko wa PSPF, LAPF, PPF na GEPF. Kufuatia hatua hii, Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) inapenda kutoa ufafanuzi katika maeneo yafuatayo:-

1.0. Kwa mujibu wa Sheria ya PSSSF Rasilimali, Mikataba iliyoingiwa na Mifuko iliyounganishwa, Mifuko ya hiari, Madeni, Rasilimali, vitega uchumi, Ofisi pamoja na akaunti za Benki za Mifuko iliyounganishwa sasa zipo chini ya Mfuko wa PSSSF.  Hivyo:- 

(i) Waajiri wote wataendelea kuwachangia wanachama/wafanyakazi wao kupitia akaunti za Benki za Mifuko iliyounganishwa hadi hapo Mfuko wa PSSSF utakapotoa maelekezo mengine.

(ii) Uandikishwaji wa wanachama wapya wanaopaswa kusajiliwa katika Mfuko wa PSSSF utaendelea kufanyika kupitia Ofisi za Mifuko iliyounganishwa hadi hapo Mfuko wa PSSSF utakapotoa maelekezo mengine.

(iii) Wanachama, Wastaafu, Wategemezi, na wadau wengine wataendelea kupata huduma zao katika Ofisi ambazo wamekuwa wakihudumiwa siku zote hadi hapo Mfuko wa PSSSF utakapotoa maelekezo mengine.

2.0. Tunapenda kuwaondoa wasiwasi Wanachama, Waajiri na Wadau wote wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii kwamba huduma zote za Hifadhi ya Jamii zilizokuwa zikitolewa na Mifuko iliyounganishwa zinaendelea kutolewa kama kawaida katika Ofisi zile zile. Endapo utahitajika ufafanuzi zaidi tafadhali wasiliana na Mamlaka (SSRA).

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano
Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
S.L.P 31846
Tovuti: www.ssra.go.tz
DAR ES SALAAM
09/08/2018

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad