HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 16 August 2018

AKINA MAMA WAJASIRIAMALI WAPATIWA KUKU 4000 WILAYANI MKURANGA

Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii

WANAWAKE wajasiriamali wapatao 400 Wilayani Mkuranga wamepewa mafunzo na kuku wa kufuga ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuendeleza shughuli za kijasiriamali Wilayani humo.


Akiongea na vyombo vya habari Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga ameeleza kuwa hadi kufikia mwakani akina mama wa Mkuranga watakuwa mbali sana kutokana na ufugaji huo wa kuku hao ambao watainua uchumi wa familia zao.

Aidha amewataka akina Mama wa Wilaya ya Mkuranga kutumia mradi huo vizuri ili kuleta maendeleo kwani wamebahatika sana.

Naye Mkurugenzi wa Wilaya ya Mkuranga Mhandisi Mshamu Munde amesema kuwa kuku hao ni kwa ajili ya ufugaji katika kujikwamua kiuchumi na sio zawadi na amewataka akina mama hao kutumia ujuzi kuendeleza ufugaji na kuwaelimisha wengine kuhusiana na mafunzo hayo.

Pia ameeleza kuwa wajasiriamali hao wamepokea kuku 1058 kati ya kuku 4000 waliohaidiwa na akina Mama 100 wamepata kuku 10 kwa kila mmoja.

Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake jukwaa la Wilayani Mkuranga bi. Mariam Ulega kuku 4000 ambao watagaiwa kwa akina mama 400 watagaiwa kwa wanawake wajasariamali waliohudhuria katika mafunzo hayo.

Ameeleza kuwa kwa hicho kidogo wakitumie katika kuleta maendeleo yao binafsi na taifa kwa ujumla, amewataka wawe na ushirikiano ili waweze kufikia malengo yao.
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filberto Sanga akizungumza leo juu ya kupoka kuku kwaajili ya  kina Mama wajasiria mali wawilhiyo iliypo mkoa wa Pwani(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Muonekano wa kuku waliopewa kina  mama wa Wilaya ya Mkuranga.

 Wakina mama wa Wilaya ya Mkuranga wakiweka kuku tatika matanga ambapo wakinamama 400 walipata kuku 10  kilammoja kwaajili wa mtaji wakufunga kuku.
Wakina mama wa Wilaya ya Mkuranga wakiweka kuku tatika matanga ambapo wakinamama 400 walipata kuku 10  kilammoja kwaajili wa mtaji wakufunga kuku.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad