HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 13 August 2018

Serikali ya Sierra Leone yatembelea bodi ya mikopo kujifunza utendaji wa bodi katika utoaji wa mikopo

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii .

SERIKALI ya Sierra Leone kupitia wizara Elimu na Ufundi na Elimu ya Juu umetembelea Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Nchini (HESLB) kujifunza na bodi hiyo inavyotoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu .

Ujio huo umekaa kwa wiki moja katika bodi hiyo ikiwa ni kuangalia namna ya kuweza kujifunza na kwenda kuanzihsa chombo hicho nchini Sierra Leone.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Nchini (HESLB) , Abdulzaq Badru amesema kuwa nchi sierra leone kufika hapo ni kutokana na umahiri katika uchakataji wa mikopo kwa wanafunzi kwa elimu ya juu.

Amesema kuwa ujumbe huo umepita katika nchi ya Ghana na kisha Tanzania kuangalia namna ya uendeshaji wa bodi katika utoaji wa mikopo.

Ujumbe huo uliongozwa na Naibu Waziri wa Elimu , Ufundi na Elimu ya Juu ya Nchini Sierra Leone Dkt. Turad Senesie , Naibu Katibu Mkuu Wizara fedha Mr. Matthew Dingie , Naibu Mkurugenzi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii na Bima Mohammed Gondoe na wajumbe wengine.

Naibu Waziri wa Elimu , Ufundi na Elimu ya Juu ya Nchini Sierra Leone Dkt. Turad Senesie amesema HESLB inafanya vizuri katika uchakataji wa mikopo na kusema kuwa wanatarajia kuanzisha chombo kama hicho nchini kwao.
Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Nchini (HESLB) , Abdulzaq Badru akizungumza na waandishi wa habari  (hawapo pichani) wakati wa kuwaaga ujumbe wa Sierra Leone waliotembelea bodi hiyo.
Naibu Waziri wa Elimu , Ufundi na Elimu ya Juu ya Nchini Sierra Leone Dkt. Turad Senesie akizungumza na waandishi habari kuhusiana na alichojifunza katika bodi ya mikopo.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad