HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 18 August 2018

SAUTI YA SHANGAZI YAZIDI KUYAFIKIA MAELFU YA MABINTI JIJINI MBEYA...

Wanafunzi wa shule ya sekondari Lyoto wapatao 800 wanufaika na Sauti ya Shangazi mara baada ya kuwatembelea Shuleni hapo, Aunty Mary Steward Mwenisongole ni Mwanamke alie jitoa kuwasaidia mabinti wa mashuleni kupunguza na kuondoa mazingira hatarishi katika ukuaji wao pindi wakiwa masomoni na wakiwa majumbani kuepuka vishawishi mbalimbali vinavyowapelekea kujiingiza katika njia zisizo sahihi zinazo pelekea kupata magonjwa ya zinaa, mimba na athali mbalimbali katika ukuaji wa Mwanafunzi.
Aunty Mary Steward Mwenisongole akizungumza na wanafunzi wakike wa shule ya sekondari lyoto iliyopo eneo la Ilemi jijini Mbeya juu ya Sauti ya Shangazi inavyo jenga kujiamini na kujikubali kwa mabinti waliopo mashuleni.
Moja kati ya mwanafunzi wa kike wa shule ya Sekondari Lyoto akichangia jambo juu ya namna ambavyo mwanamke anatakiwa kujiamini na kujikubali pindi awapo shuleni na nyumbani kwa kupitia muongozo mzuri wa Sauti ya Shangazi.
Licha ya Aunty Mary kufika shuleni hapo ilimjengea imani kubwa ya kuamini juu ya mabadiliko makubwa aliyoanza kuyaona tangu siku hiyo ya kwanza kufika katika shule hiyo na kupelekea ushawishi wa kutunuku zawadi mbalimbali kwa mabinti wa shule hiyo ya lyoto Sekondari iliyopo ndani ya jiji la Mbeya.
Moja kati ya waalimu wakifuatilia mafunzo kwa umakini juu ya namna ambavyo Sauti ya Shangazi Inaweza Kuwasaidia Mabinti Kuepukana na changamoto Mbalimbali..
Hakika mabinti wa shule ya Lyoto Sekondari hawakujutia maana Sauti ya Shangazi Iliwajengea Uwezo na Kujiamini. Anko T, akitoa mada kwa mabinti juu ya walipotoka, walipo na wanapotaraji kufika..Picha na Mr.Pengo Mbeya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad