HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, 19 August 2018

Bonanza la mpira wa miguu kwa timu za wasichana shule za sekondari na msingi manispaa ya Kigoma ujiji lafana sana


Bonanza mpira wa miguu kwa timu za wasichana kwa shule za sekondari na msingi limefanyika jana katika manispaa ya Kigoma ujiji, Mkoani Kigoma. Jumla ya timu nane zilichuana vikali ambapo timu ya Shule ya msingi Klasta ya Kigoma Kaskazini iliibuka mshindi kwenye mashindano hayo.
Lengo la bonanza hilo ilikuwa ni kuwezesha watoto wakike katika kukuza vipaji na kugundua vipaji vipya  vya watoto wa kike, lililoratibiwa na Muwakilishi UWT Mkoa wa Kigoma, Miriam Ntakisivya (kushoto pichani) ambalo litakua ni muendelezo kila baada ya miezi kadhaa, bonanza hili limedhaminiwa na radio Joy 90.5 Kigoma, Riam Bookstore pamoja na Tanganyika Water. anayeonekana kushika kipaza sauti ni Mkurugenzi wa radio Joy 90.5 Kigoma, Mwenge Muyombi alipikuwa akizungumza na wanafunzi hao katika ufunguzi wa Bonanza hilo.
Sehemu ya wageni waliofika kwenye Bonanza hilo wakifatilia michezo hiyo.
Picha ya pamoja.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad