HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 9 July 2018

Wizara ya Ardhi Yaahidi Ushirikiano Kwa Naibu Katibu Mkuu Mpya

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dorothy Mwanyika akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu  mpya wa Wizara hiyo Bw. Mathias Bulugulu (kushoto) na kumuaga Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka(kulia) ambaye awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu katika wizara hiyo leo Jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu  ofisini Naibu Katibu Mkuu  wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Mathias Bulugulu (aliyekaa mbele kushoto) na kumkabidhi vitendea kazi leo Jijini Dodoma. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bibi. Dorothy Mwanyika.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Mathias Bulugulu akielezea jambo wakati wa hafla fupi ya kukaribishwa kwake katika ofisi za Wizara hiyo leo Jijini Dodoma.Kutoka kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka ambaye awali  alikuwa Naibu wa Wizara hiyo, katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bibi. Dorothy Mwanyika.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dorothy Mwanyika(katikati) na Naibu Katibu Mkuu  mpya wa Wizara hiyo Bw. Mathias Bulugulu (kushoto) wakifurahia jambo mara baada ya kumkabidhi zawadi ya ua kwa ajili ya pongezi na kumuaga Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusilukaambaye awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu katika wizara hiyo leo Jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dorothy Mwanyika(katikati) akimkabidhi zawadi na Naibu Katibu Mkuu  mpya wa Wizara hiyo Bw. Mathias Bulugulu (kushoto) katika hafla fupi ya mapokezi yake na kumuaga aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo ambaye sasa amekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka (kulia) leo Jijini Dodoma.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Bibi.  Dorothy Mwanyika akimpongeza Naibu Katibu Mkuu  mpya wa Wizara hiyo Bw. Mathias Bulugulu mara baada ya kumkaribisha rasmi katika ofisi za wizara hiyo Jijini Dodoma leo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Bibi.  Dorothy Mwanyika akimpongeza Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Fedha wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),Bw. Ndossi wakati wa hafla ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu  mpya wa Wizara hiyo Bw. Mathias Bulugulu leo Jijini Dodoma. Katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka ambaye awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
 Mthamini Mkuu Tanzania toka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Evelyne Mugasha akitoa neno la shukrani kwa na ukaribisho  wakati wa hafla fupi ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Mathias Bulugulu( waliokaa mbele kushoto) na kumuaga aliyekuwa Naibu wa Wizara hiyo ambaye sasa amekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka(kulia) leo Jijini Dodoma.Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bibi. Dorothy Mwanyika.
 Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji toka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. John Lupala akitoa neno wakati wa hafla fupi ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Mathias Bulugulu(kushoto) na kumuaga aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ambaye sasa amekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka(mwenye miwani) leo Jijini Dodoma. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bibi. Dorothy Mwanyika.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Dkt. Moses Kusiluka ambaye awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akipongezana na Naibu Katibu Mkuu  mpya wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Mathias Bulugulu mara baada ya kumkabidhi rasmi ofisi na vitendea kazi katika hafla fupi iliyofanyika katika Ofisi za Wizara hiyo Jijini Dodoma leo.(Picha zote na: Frank Shija - MAELEZO, Dodoma)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad