HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 9 July 2018

BENKI YA KCB TANZANIA YAZINDUA TAWI LAKE JIPYA LA MBAGALA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Benki ya KCB Tanzania imefanya uzinduzi wa tawi lake la 14 lililopo Mbagala jijini Dar es salaam. Tawi hilo limezinduliwa rasmi na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mh. Dkt Ashatu Kijaji akiwa ameambatana na Mbunge wa Mbagala Issa Mangungu.

Dkt Ashatu  amesema kuwa amefurahishwa na utendaji kazi wa benki ya DCB ndani ya miaka mitano ikiwemo ulipaji wa kodi na jumla ya Bilioni 40 imelipwa kama kama cooperate Tax na kodi nyinginezo.

Amesema kuwa KCB imeshirikiana na serikali katika utekelezaji wa miradi ikiwemo ujenzi wa barabara na majengo mbalimbali, udhamini waligi kuu ya soka Tanzania ikiwa ni lengo la kuinua sekta ya michezo.

Katika uzinduzi huu Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Zuhura Muro aliweza kusena baadhi ya mafanikio machache ambayo KCB imeweza kufanya kwa jamii. 

Amesema Benki KCB  imewezesha miradi mikubwa ya maendeleo ya nchi yetu kutokana na rasilimali za KCB Group (strong balance sheet) ambapo Miradi hiyo ni kama Barabara ya Msata hadi Bagamoyo, Ujenzi wa Terminal Three (3) JNIA, jengo la One stop Centre TPA na Emergency Laboratory Building (Ofisi ya Raisi, Makumbusho) kwa kutaja tu michache.

Alisema, “Ndugu mgeni rasmi natumaini unakumbuka vizuri mwaka 2017 uliitikia wito wa kuwa mgeni rasmi kwenye warsha ya 2jiajiri iliyokutanisha wanawake zaidi ya 1500 hapa jijini Dar es salaam. Leo nina furaha kurudisha mrejesho kuwa baada ya kutambua mahitaji ya kifedha ya wanawake wajasiriamali, KCB Banki imeshazindua “2jiajiri Women Account” amabayo inawawezesha kuweka akiba na kupata mikopo kwa masharti mepesi na rafiki. Ulitupa changagmoto nasi tukaifanyia kazi.”

Wazungumzaji walisisitiza kuwa Tawi hili la Mbagala ni sehemu ya jitihada za kuweza kufikia wateja wao wengi lakini pia kutanua wigo wa huduma za kibenki. 

Wazungumzaji waliwakaribisha wakazi wote wa Mbagala na wakaribu kutumia huduma zao za kibenki na kufahamu zaidi faida zitokanazo na kuwa mteja wa KCB Bank ikiwemo mikopo, akaunti za akiba zenye faida lukuki, mtandao mkubwa wa ATM zaidi ya 962 Afrika mashariki.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkurugenzi mtendaji wa KCB Bank Bw. Cosmas Kimario alisema benki hiyo inaunga mkono jitihada za serikali katika kuleta maendeleo kwa wananchi kwa kuboresha huduma zetu ili kuendana na kasi ya mabadiliko na ukuaji wa uchumi.

Vilevile Mkurugenzi Mtendaji aliendelea kusema, kipindi cha kota ya kwanza ya 2018 benki hiyo imeweza kupata faida ya shilingi Bilion 3.6/- benki imeweza kuthibiti madeni chechefu (NPL) kufikia asilimia 7% kiwango ambacho ni kizuri katika utendaji wa kibenki.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Benki KCB Zuhura Muro akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi la Benki hiyo Mbagala leo Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa KCB benki na Mbunge wa Mbagala Ally Mangungu baada ya uzinduzi wa tawi la Benki ya KCB Mbagala uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji akisaini kitabu cha wageni. 
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji akizindua tawi la Benki ya KCB Mbagala akiwa pamojpana Mkurugenzi Mtendaji Cosmas Kimaro na Mwenyekiti wa Bodi Zuhura Muro leo Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji akikata utepe baada ya kuzindua tawi la Benki ya KCB Mbagala leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji akizungumza na wananchi waliojitokeza pamoja na viongozi wa Benki ya KCB wakati wa uzinduzi wa tawi la Mbagala Leo Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad