HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 9 July 2018

Wachimbaji Wadogo Kunufaika na Vituo Vya Umahiri

Waziri wa Madini Mhe.Angellah Kairuki akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kusaini mikataba mitatu ya ujenzi wa vituo saba vya umahiri pamoja na jengo la mafunzo kwa wachimbaji wadogo katika chuo cha Madini Dodoma. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo, Kulia ni Katibu Mkuu Wizara hiyo Prof Simon Msanjila  na Mkurugenzi Mtendaji wa Idara ya Ujenzi-SUMA JKT Mhandisi Morgan Nyonyi. 
Katibu Mkuu Wizara Wizara ya Madini Prof Simon Msanjila(kushoto)  na Mkurugenzi Mtendaji wa Idara ya Ujenzi-SUMA JKT Mhandisi Morgan Nyonyi wakibadilishana mkataba wa ujenzi wa vituo saba vya umahiri pamoja na jengo la mafunzo kwa wachimbaji wadogo  na vitakavyojengwa  katika  chuo cha Madini Dodoma. 
Waziri wa Madini Mhe.Angellah Kairuki na Naibu Waziri wake Mhe. Stanslaus Nyongo wakishuhudia utiaji saini mikataba mitatu ya ujenzi wa vituo saba vya umahiri pamoja na jengo la mafunzo kwa wachimbaji wadogo vitakavyojengwa  katika chuo cha Madini Dodoma.Wanaotia saini ni Katibu Mkuu Wizara hiyo Prof Simon Msanjila  na Mkurugenzi Mtendaji wa Idara ya Ujenzi-SUMA JKT Mhandisi Morgan Nyonyi. Picha zote na Daudi Manongi-MAELEZO,DODOMA. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad