Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
Waziri wa maji na Umwagiliaji,
Profesa Makame Mbarawa amesema hatamfumbia macho mfanyakazi atakayezembea
kazini kwa namna yoyote badala yake atamsafisha mara moja na kumtoa kabisa
kwenye idara na kumuhamishia hata chuoni.
Profesa Mbarawa ameyasema hayo
leo wakati alipotembelea ofisi za Dawasa zilizopo Mwanayamala jijini Dar es
Salaam.
“Tunataka kufanya maendeleo, sitamtoa mtu kwa kumuonea nikikuona
wewe umekaa pale na miradi yetu uliyochelewesha nitakuacha, kwa nini nikuache, najua utafanya vile vile,
na sitakuacha kwenye idara, nitakupeleka chuo cha maji, si kwa ajili ya
kuwakomesha wanafunzi hapana, ila sitamuacha mtu aliyefanya ujinga aendelee”.
Amesema, uteuzi huu ni heshma kubwa kwani sasa anakwenda moja kwa
moja kutatua matatizo ya watanzania ambao hasa ukienda vijijini ndio utajua
kuwa kuna watanzania wana shida ya maji.
Amewaasa wafanyakazi hao kuwa na lengo la pamoja la kuhakikisha
wanamsaidia Mtanzania yule masikini, kuweza kupata maji
“Tunasema tumtue mama
ndoo kichwani kwa kumpelekea maji karibu”.
“Ninaamini tukiungana wote kwa pamoja tutaweza, hakuna jambo
lisilowezekana, muhimu ni kujipanga na kuwa na nia thabiti ya kuwasaidia
watanzania kupata maji.
Akizungumzia kuhusi muunganiko wa Dawasa na Dawasco, amesema suala
hilo litafanyika haraka sana kwani liko kisheria, limeenda bungeni na sheria
imetungwa kuwa pamoja.
Aliongeza kuwa uunganishwaji wa taasisi hizo mbili umefanywa kwa
nia njema na kuleta ufanisi mkubwa, kwani kwa kufanya hivyo ufanisi wa kazi
utaongezeka zaidi kuliko kama wangelikuwa vipande vipande viwili. Na pia
wataongeza nguvu na kufanya kazi vizuri zaidi.
“Majina ya CO nayajua
nimeletewa majina ya mwenyekiti wa bodi yameishapelekwa kwenye bodi yenye
mamlaka na leo nimeitisha majina ya wanachama wa bodi ambayo baada ya wiki
mbili tatu nitayajua nitayapeleka kwenye veti, ili tuwe kitu kimoja twende
mbele.
Ameongeza kuwa, hakuna
mfanyakazi yeyote kutoka Dawasa ama Dawasco atakayepoteza kazi kutokana
na muunganikano huo isipokuwa kwa yule mzembe ama mwizi.
Amesema ni lazima pia kwa
muunganiko huo ambao unaifanya Taasisi kuwa moja kuwa na malengo, ambapo lengo
la kwanza ni kumpelekea mtanzania maji.
Aidha Profesa Mbarawa amewataka
Dawasa kuhakikisha wanaongeza wateja wa maji kwa kipindi cha mwaka mmoja kutoka
Wateja wadogo wadogo waliopo sasa takribani 264,000 hadi kufikia 850,000
“Dawasa lazima tutengeneze wateja 850,000 naimani tunaweza,
na mkifanya hivyo mapato yatafikia mapaka bilioni 600 na 700. Twende tukatafute
wateja, wateja wapo wengi, amesema Mbarawa.
Aidha Profesa Mbarawa Katika hatua nyingine waziri huyo alitoa wito kwa Dawasa kuanza
mchakato wa kutumia mita za mfumo wa kulipia kabla kama alivyokuwa amewaagiza
kipindi alipokuwa waziri wa wizara hiyo mwaka 2015 jambo ambalo halikufanyika.
Pia amewaasa wafanyakazi kuwa waadilifu kazini na kuwa na
mawasiliano mazuri hususani mawasiliano kati ya wafanyakazi wa chini na uongozi
wa juu kila mfanyakazi ajue nini kinafanyika ili awe sehemu ya kazi, kama ni
mradi basi awe sehemu ya mradi. 

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa akisalimiana na wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), wakati akiwasili kuzungumza nao makao makuu ya mamlaka hiyo, Dar es Salaam leo.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) leo alipotembelea makao makuu ya mamlaka hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wakimsikiliza Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa alipotembelea ofisini hapo leo.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa(kushoto) akizungumza na Mkurugenzi wa DAWASCO Mhandisi Cyprian Luhemeja alipotembelea katika ofisi za DAWASA leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa akiagana na wafanyakazi wa DAWASA mara baada ya kumaliza ziara yake katika ofisi za mamlaka hiyo.
No comments:
Post a Comment