HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 4, 2018

COSOTA YAWATAKA WASANII KUSAJILI KAZI KWA MANUFAA YAO

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


CHAMA cha Hakimiliki Tanzania COSOTA kimewataka wasanii wa filamu na muziki kutambua umuhimu wa kusajili kazi zao kabla ya kuzipeleka sokoni au kuuza kwa makampuni makubwa.

Hayo yamesemwa na COSOTA leo katika Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea ndani ya Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.



Akizungumza na Globu ya Jamii, Afisa Hakimiliki na Leseni Ngutunyi David amesema wasanii wengi sana walishindwa kunufaika kwa kazi walizozifanya kutokana na kuuza kazi zao kwa makampuni makubwa ambayo yanakuja kufaidika kwa muda mrefu.

Ngutunyi amesema, msanii anashindwa kuelewa kuwa unapouza kazi yako kwa kampuni kubwa na kupewa kiasi kikubwa cha hela kwa wakati mmoja hakiwezi kuja kukusaidia baadae na kuacha watu wengine wakifaidika kwa muda wote.

Akielezea umuhimu wa kusajili na kupata hakimiliki kwa kazi wasanii, Ngutunyi amesema msanii anaposajili kazi yako inakupa nguvu ya kudai maslahi yako pindi pale mtu anapokuja kutengeneza au kubuni kitu kama cha kwako.

"Msanii anapokuja COSOTA na kusajili kazi zake zinampa nguvu ya kudai maslahi pindi pale mtu anapokua amenakili kazi yako kwa kupeleka malalamiko na sisi kama watoaji hakimiliki tunamuita na kukaa chini kwa ajili ya majadiliano,"amesema Ngatunyi.

"Malalamiko yamekuwa mengi sana kwa wasanii hususani wa filamu wameshindwa kunufaika na kazi zao baada ya kuziuza kwa makampuni makubwa na sasa wamepata matatizo wanakosa msaada,"amesema Ngutunyi.

Mbali na wasanii wa filamu na muziki, Ngatunyi amewataka waandaaji wa vipindi mbalimbali vya redio na televisheni kusajili kazi zao ili kuepukana na suala la kazi kuingiliana.

COSOTA inafanya kazi ya kutoa leseni na hakimiliki kwa wasanii wa aina mbalimbali na waandaaji wa vipindi na wamewashauri wasanii kufuata taratibu za usajili kwa kazi zao ili ziwanufaishe kwa kipindi kirefu.
Mtoa huduma COSOTA upande wa Kumbukumbu Aneth Maimu akizungumza na Globu ya Jamii  akiwa pamoja na Afisa Hakimiliki na Leseni Chama cha Hakimiliki COSOTA Ngutunyi David (kushoto)  akielezea umuhimu wa wasanii kusajili kazi na kuacha kuuza kwa makampuni makubwa.Picha na Emmanuel Massaka.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad