HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 4 July 2018

TANCDA YATOA HUDUMA YA USHAURI NA UPIMAJI WA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA BURE KATIKA MSIMU WA SABASABA

Na Leandra Gabriel, Globu ya Jamii.


SHIRIKISHO la vyama vya magonjwa yasiyoambukiza (TANCDA) linalojihusisha na utoaji wa elimu ya afya, ushauri na upimaji wa magonjwa ya yasiyoambukiza imepiga kambi katika viwanja vya sabasaba wakihudumia wananchi bure kabisa.


Akizungumza na Michuzi blogu Meneja mradi wa shirikisho hilo bi. Happy Nchimbi ameeleza kuwa katika maadhimisho hayo ya sabasaba wanatoa huduma kwa wananchi bure kabisa ikiwemo kutoa elimu juu ya magonjwa yasiyoambukizwa.

Aidha ameeleza kuwa wanapima magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza ikiwemo kisukari, shinikizo la damu na uwiano wa uzito na urefu bure kabisa.

Pia ameeleza kuwa wanatoa ushauri kuhusiana na mtindo bora wa maisha hasa katika kuepukana na magonjwa hayo yasiyo na maambukizi.

Huduma hiyo imeanza kutolewa kuanzia Julai 2 mwaka huu na yatamalizika Julai 7 na kuendelea kutolewa bure katika hospitali ya taifa ya Muhimbili katika jengo la kliniki ya kisukari kwa ushauri na upimaji.
Watoa huduma wa afya katika banda la Shirikisho la Vyama vya magonjwa yasiyo ya kuambukiza TANCDA wakitoa huduma kwa wananchi waliojitokeza kwa ajili ya kupata huduma za upimaji wa afya kwa magonjwa kwa yasiyo ya kuambukiza kwenye maonyesho ya 42 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea ndani ya Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es salaam.
Meneja mradi wa Shirikisho la Vyama vya magonjwa yasiyo yakuambukiza TANCDA Happy Nchimbi akizungumza na Globu ya Jamii akielezea huduma wanazozitoa kwenye banda lao kwenye maonyesho ya 42 ya kimataifa ya biashara ndani ya Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mauzo wa Kampuni ya Belva Consult Elizabeth Charles akimkabidhi Under Pad mwana Globu ya jamii alipotembelea banda lao ndani ya maonyesho ya maonyesho ya 42 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam. Picha na Emanuel Massaka.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad