HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 10 July 2018

MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO WAANZA KUTEKELEZA MKAKATI WA KUSHIRIKIANA NA WADAU WA UTALII

Na Ripota Wetu, Arusha 
MAMLAKA ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), imeanza kutekeleza mkakati wa kushirikishana na wawekezaji waliopo sekta ya utalii ili kubaini maeneo mapya yanayofaa kwa uwekezaji kwenye hifadhi hiyo.

Wajumbe wa Menejimenti ya NCAA wamefanya ziara ya kutembelea maeneo hayo yanayofaa kuwa uwekezaji katika huduma tofauti ikiwamo hoteli, kambi, utalii wa magari ya waya maeneo ya bonde la Ngorongoro na Embakai.

Chini ya uratibu wa Mpango wa matumizi bora (GMP), imeelezwa kwamba maeneo haya yataongeza makusanyo ya mapato kutokana na shughuli za utalii kwenye mamlaka ya hifadhi hiyo.

Akizungumza kwenye ziara hiyo Naibu Mhifadhi wa mamlaka hiyo Asangye Bangu alisema, ziara hiyo imelenga kuangalia maeneo yanayofaa kwa uwekezaji  kama hoteli,kambi za muda za kulala wageni ,utalii wa baluni na biashara nyingine ndani ya hifadhi ikiwamo kuhakikisha wanakuwa na mpango endelevu wa uhifadhi,utalii na jamii inanufaika

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala nchini (TATO), Wilbard Chambulo akizungumzia ushirikishwaji huo wa sekta binafsi aliipongeza Mamlaka hiyo kwa kushirikisha wadau waliopo kwenye sekta hiyo

Baadhi ya  maeneo ambayo jopo hilo la wawekezaji liliyatembelea ni pamoja na nakumbusho ya  Olduvai Gorge,Nasera rock,Ndutu na maeneo mengine.
 Naibu Mhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro Asangye Bangu akizungumza na wafanyabiahara wawekezaji waliofanya ziara ya kujionea maeneo mapya ya uwekezaji kwenye hifadhi hiyo. 
 Naibu Mhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro (NCAA) Asangye Bangu kulia, akizungumza na wafanyabiahara wawekezaji waliofanya ziara ya kujionea maeneo mapya ya uwekezaji kwenye hifadhi hiyo.  
 Wawekezaji na baadhi ya wafanyakazi wa Hifadhi ya Ngorongoro wakijadiliana baadhi ya masuala ya utalii pembeni mwa kivutio cha mwamba wa Nasera Rock kinavyopatikani hifadhin humo.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Utalii nchini (TATO), Wilbard Chambulo akiwaonyesha wawekezaji wenzake pamoja na maofisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro baadhi ya maeneo yanayozunguka kivutio cha Nasera Rock.
 Baadhi ya wawekezaji waliotembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wakimsikiliza Naibu Mhifadhji Asangye Bangu.
 Naibu Mhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro (NCAA) Asangye Bangu kulia, akizungumza na viongozi wa Chama cha Mawakala wa Utalii nchini (TATO) wakati wa ziara ya kutembelea na kujionea maeneo mapya ya uwekezaji kwenye hifadhi hiyo.
 Kundi la wawekezaji wakimsikiliza Naibu Mhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro Asangye Bangu wakati wa ziara yao ya kujionea maeneo mapya ya uwekezaji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad