HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 10 July 2018

WANAYANGA WALIA NA ABBASI TARIMBA

Na Agness Francis, Globu ya Jamii

WANAYANGA wamechukizwa na kitendo cha Mwenyekiti wa Kamati ya Yanga Abbasi Tarimba kuzungumza habari za klabu hiyo zisizokuwa na uhakika kwenye kituo cha redio.

Ambapo wamedai kuwa Mwenyekiti  huyo ameongozana mpinga maendeleo wa Yanga Mohammedi Msumi kwenda redioni,ikiwa walichotegemea  kutoka kwake ni kuelezea ameifanyia nini klabu hiyo toka alivyochaguliwa Juni 10 mpaka leo Julai 10 mwaka huu.

Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es  Salaam  Mwenyekiti wa  matawi ya klabu ya yanga Tanzania Bakili  Makele amesema  kuwa fedha za Sportpesa  zinatoka kwa mujibu wa mikataba na si kwa matakwa ya Tarimba kama anavyojinasibu kuwa amelipa wachezaji,ikiwa hakuna fedha yake yoyote  iliyopokelewa klabuni.

Makele amekanusha kuwa hakukuwa na taarifa ya kuvunjwa  kwa kamati hiyo ya Tarimba katika mkutano wao uliofanyika,ingawa  wanachama hao walileta hoja hiyo mezani

Makele amesema katika hoja hiyo Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga alikataa na kwa kuwa hakuwa na majukumu ya  kuvunja mamlaka ya mkutano mkuu.

"Tunasikitika kwa hesmima ya Tarimba  hapaswi kukurupuka kama anavyopokea taarifa kwa akina msumi na kuzifanyia maamuzi,sasa tunaamini adui mwingine wa maendeleo ya klabu ya yanga ni yeye,amesema Makele.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad