HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 3, 2018

Wateja Halopesa sasa kutuma pesa bure

·       Sasa wataweza kutuma na kupokea pesa kutoka mitandao mingine.
 Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel imeondoa gharama za kutuma pesa kwa wateja wanaotumia huduma ya kifedha ya Halopesa, na hivi sasa wataweza kutuma pesa bure Halopesa kwenda Halopesa, huku pia ikipunguza gharama za kutuma fedha kutoka Halopesa kwenda mitandao mingine.
Kuondolewa kwa makato hayo inatafsiriwa na kampuni hiyo kama njia pekee ya kupanua wigo wa huduma za kifedha kwa mamilioni ya Watanzania ambao wanatumia huduma za kifedha kwa njia ya simu.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Halopesa, Vu Tuan Long, amesema kuwa kuondolewa kwa gharama hizo kutawezesha wateja wa mtandao huo hasa walioko katika maeneo ya vijijini kuweza kufanya miamala ya simu na kuondokana na usumbufu ambao wangeweza kuepuka kwa kutumia njia nyingine kutuma fedha ili kuokoa gharama za makato ya kufanya miamala.
“Tuna mamilioni ya watanzania ambao kwa mara ya kwanza walipata mawasiliano ya simu tulipoanzisha huduma zetu, na baada ya kuanzishwa kwa huduma ya Halopesa kwa miaka miwili sasa wateja wetu katika maeneo mbalimbali wanaweza kutuma pesa bure Halopesa kwenda Halopesa,” Alisema Long na kuongeza.
“Hii ni hatua nyingine ya kuhakikisha kwamba wateja wanakuwa na wigo mkubwa wa kuweza kukidhi mahitaji yao katika nyanja mbalimbali za kiuchumi, na kijamii kupitia huduma ya kifedha ya mtandao kwa ubora, ukaribu, uhakika  na usalama zaidi na kuepuka kwenda umbali mrefu kwaajili ya kufuata huduma za kifedha kupitia benki”. Aliongeza Long.
Aidha Mkurugenzi huyo, alibainisha kuwa, licha ya kuondoa gharama katika kutuma fedha, huduma ya kutuma fedha kutoka Halopesa kwenda mitandao mingine imepunguzwa gharama ili iwe rahisi zaidi kwa wateja wanaotuma pesa kwenda mitandao mingine ya simu pia waweze kutuma pesa kwa gharama nafuu.
“Habari njema tuliyonayo kwa wateja wetu ni kuwezeshwa kwa huduma ya Halopesa kuweza kutuma pesa kwenda mitandao yote, sasa wateja wetu wataweza kutuma pesa kwenda mitandao mingine kwa gharama nafuu zaidi kabisa,” Alihitimisha Long
Tangu kuanzishwa kwa huduma ya Halopesa tayari Mawakala Zaidi ya elfu 55,000 tayari wamejisajili na wanatoa huduma kwa zaidi ya wateja milioni moja na nusu walioenea nchi nzima.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel Nguyen Van Son pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni hiyo,Mhina Semwenda wakifungua shampeni kuashiria uzinduzi wa huduma ya wateja wa Halopesa kutuma pesa bure Halopesa kwenda Halopesa, wanaoshuhudia ni Mkuu wa kitengo cah Halopesa Vu Tuan Longa (Kulia) na Meneja biashara wa Halopesa Magesa Wandwi (Kushoto). 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel Van Nguyen Son pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni hiyo,Mhina Semwenda wakishika glasi za shampeni katika uzinduzi wa huduma ya wateja wa Halopesa itakao wawezesha kutuma pesa bure Halopesa kwenda Halopesa, wanaoshuhudia ni Mkuu wa kitengo cah Halopesa Vu Tuan Longa (Kulia) na Meneja biashara wa Halopesa Magesa Wandwi (Kushoto).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel Van Nguyen Son pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni hiyo,Mhina Semwenda pamoja wa wafanyakazi wengine wa Halotel wakigonga glass za shampeni kuashiria uzinduzi wa huduma ya wateja wa Halopesa itakao wawezesha kutuma pesa bure Halopesa kwenda Halopesa, wanaoshuhudia ni Mkuu wa kitengo cah Halopesa Vu Tuan Longa (Kulia) na Meneja biashara wa Halopesa Magesa Wandwi (Kushoto).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad