HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 6 July 2018

VETA YAJIPANGA KUTOA UJUZI KATIKA SEKTA YA VIWANDA

Na Chalila Kibuda Globu ya Jamii
MAMLAKA ya Elimu  na Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA) imesema kuwa wamejipanga katika utoaji wa elimu ufundi katika uchumi wa viwanda.

Akizungumza mara baada ya kupokoea kikombe cha ushindi Mwenyekiti wa bodi ya VETA, Peter Maduki amesema kuwa dhamira ya VETA ni kuhakikisha viwanda vinapata ujuzi unaotoka VETA.

Amesema kuwa kumekuwa na mafanikio katika utoaji wa mafunzo ya ufundi stadi ikiwa nipamoja vijana kuingia katika soko la ajira za moja kwa moja na wengine wakijiajiri .

Maduki amesema katika uchumi wa viwanda VETA ina nafasi kubwa hivyo  ni wajibu wao kuzalisha vijana wengi wa kutumika katika uchumi huo na taifa kusonga mbele .

Aidha ametoa wito wa vijana kujiunga na vyuo vya VETA katika kupata ujuzi na kuwa watu kuzalisha pamoja na kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao.

“Hatutarudi nyuma kwa kuliacha jambo la viwanda wakati ni sehemu ya wadau muhimu wa katika utoaji wa ujuzi wa viwanda”
.Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano Watanzania, Kassim Majaliwa akikabidhi kikombe cha ushindi kwa Mwenyekiti wa Bodi wa VETA, Peter Maduki katika ufunguzi wa maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi wa VETA, Peter Maduki akitoa maelezo katika banda la Chuo Kikuu Mzumbe wakati alipotembelea banda hilo katika maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Bodi wa VETA, Peter Maduki akipata maelezo katika banda la Chuo Kikuu Mzumbe wakati alipotembelea maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Bodi wa VETA, Peter Maduki akipata maelezo katika banda DIT wakati alipotembelea banda katika maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mteja wa akipata maelezo ya kusoma Kipawa VETA kwa njia ya mtandao wakati alipotembelea banda katika maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mwanafunzi wa VETA kipawa akitoa maelezo ya ubunifu wa uzio wa ulinzi kwa mwananchi aliyepotembelea banda katika maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa VETA wakiwa katika furaha ya ushindi wa kikombe katika maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad