HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 6 July 2018

NAIBU WAZIRI NDITIYE AITAKA TCRA KUWACHUKULIA HATUA KAMPUNI ZA VING’AMUZI KWA KUACHA KURUSHA MATANGAZO YA BURE


Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Malaba akizungumza kuhusiana na utendaji wa TCRA katika utoaji wa huduma za mawasiliano nchini.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
NAIBU Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Nchini (TCRA) kuwachukulia hatua kampuni za ving’amuzi kutokana na kuacha kurusha matangazo ambayo yako kwa mujibu wa leseni zao.

Nditiye ametoa agizo hilo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu iliyotembelea Mamlaka hiyo , amesema watoa huduma za ving’amuzi wanatakiwa kutoa matangazo bure hata kama mtu hajalipia.

Amesema kuwa TCRA ifuatilie na kama kampuni za ving’amuzi zitaendelea kutoonyesha matagazo bure katika vituo vitano vya luninga wawafungie kutokana na ukiukaji wa leseni walizoombea.

Vituo ambavyo vinatakiwa kurusha matangazo bure bila kulipia ni ITV, Chanel Ten, Star TV,EATV pamoja na Clouds.

Nditiye amesema kuwa maoni kamati watayafanyia kazi katika kupata ufumbuzi ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.

Amesema kuwa sekta ya mwawasiliano ni ya pili katika uchangiaji wa pato la Taifa ambapo mawasiliano inachangia asilimia 13.1.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Suleimani Kakoso amesema kuwa TCRA lazima ijipange katika teknolojia kutokana na kubadilika kila siku.

Amesema kuwa kadri ya mabadiliko ya Teknolojia yanavyoendelea kukua baadhi ya watu wanajifunza namna ya kufanya wizi kwa kutumia teknolojia.
Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza na kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu iliyotembelea Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA).
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Suleimani Kakosoa kuhusiana na kamati iliyoyaona na kutaka ikiwa ni kwa ajili ya TCRA kuendelea kufanya vizuri katika mawasiliano.
Baiskeli iliyokuwa ikitumika Shirika la Posta katika kusambaza barua.

Moja ya Huduma mawasiliano iliyokuwa ikitolewa na TTCL ya kupiga simu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad