HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 6 July 2018

DAWASA yatekeleza miradi ya kuondoa kero za maji kwa wananchi

Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.
Mamlaka ya maji safi na maji taka (Dawasa) inatekeleza mradi Mkubwa wa upanuzi wa chanzo cha maji Chalinze ili kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa maji kwa wakazi wa mkoa wa pwani.

Mradi huo ambao kwa sasa uko katika hatua ya tatu  utahakikisha pia upatikanaji wa maji katika viwanda unakuwa wa uhakika.

Akiongea katika ziara  ya kukagua.. Maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maji na upanuzi wa chanzo cha mtandao wa maji Chakinze, waziri wa maji na umwagiliaji, Profess Makame Mbarawa.amewahakikishia wawekezaji nchini kuwa jitahada kubwa zinafanywa kuhakikisha upatikanaji wa uhakika wa maji katika viwanda vyote kikiwemo cha Sayona.

Amesema, Dawasa kama sekta ya maji, watahakikisha wanatekeleza  azma ya kumaliza tatizo kubwa la maji hadi kwenye viwanda, kwani hakuna kiwanda kitakachoendelea bila ya kuwa na maji ya kutosha.

Naomba niwahakikishie watanzania wenzangu ambao wanania thabiti ya kujenga viwanda kwa ajili ya kukuza uchumi wetu, sisi kama sekta ya maji tutahakikisha kwamba tunawapa nguvu zetu zote na kuwawekea miundombinu ya kisasa ili huduma ya maji iweze kuwafikia na waweze kufanya kazi zao za uzalishaji ili nchi yetu iweze kukua kufikia uchumi wa wakati 2025" amesema Mbarawa.

Aidha ameongeza, katika kutekeleza hilo tayari kuna mradi wa kupeleka maji kwenye kiwanda kikubwa cha Sayona ambao utahusisha kuuweka bomba la maji kutoka kwenye vyanzo vya maji mpaka kufikia kwenye kiwanda hicho, umbali wa kilometa 70 ujenzi ambao  utagarimu shilingi milioni 12

Wakati huohuo waziri Mbarawa amemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi wa Chalinze kuhakikisha unakamilika mwishoni mwa mwezi November mwaka huu. 

Amesema serikali haitasita kuwachukulia hatua wakandarasi wanaochelewesha miradi kwani lengo la serikali ni kupeleka Huduma  bora ya maji kwa wananchi.

Mradi huo wa Chalinze utahusisha upanuzi wa mtambo wa kusafisha maji wa Chalinze ambao chanzo chake ni mto Wami, lengo kubwa likiwa ni kuongeza uzalishaji kufikia Mita za ujazo 900 kwa saa kutoka mita za ujazo 500.

Mradi huo ambao mpaka utakapokamilika utagarimu USD 41,362023.43 ambazo ni mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya India kupitia Exim benki utahusisha pia ujenzi wa matanki 19,ulazaji wa mabomba ya ukubwa mbali mbali ya umbali wa kilometa 1022, ujenzi wa vizimba 351  vya kuchota maji katika vijiji na vitongoji vya Bagamoyo na Chalinze huku vizimba vingine vinatarajiwa kujengwa katika baadhi ya maeneo ya halmashauri za Handeni, Tanga na Ngerere mkoani Morogoro.

"Mradi huu ukikamilika wakazi wa pwani na Dar es Salaam watafadika na kusahau kabisa kero ya maji.
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na watumishi wa Chaliwasa, wilaya ya Chalinze mkoani Pwani kabla ya kukagua mradi wa uboreshaji upatikanaji Maji Chalinze.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa akiangalia mchoro wa ramani ya mradi huo, Chalinze.

 Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa, akikagua mradi wa uboreshaji miundombinu ya maji , Chalinze mkoani Pwani. 
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa akitoa maagizo kwa mkandarasi OIA Overseas Infrustrature Alliance mara baada ya kumaliza ya kukagua mradi wa uboreshaji upatikanaji Maji Chalinze.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad