HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 6 July 2018

GRACE PRODUCTS ATAJA SABABU ZA KUTWA TUZO YA THE INTERNATIONAL QUALITY SUMMIT AWARDS

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MSHINDI wa tuzo ya The International Quality Summit Award amewataka watanzania kupenda vitu vya nyumbani kwa sababu ni bidhaa zinazotengenezwa kwa malighafi asili na kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ya Tanzania kwenda uchumi wa Viwanda.

Mwishoni mwa Mwezi wa June,Dr Elizabeth Kilili aliweza kunyakua tuzo ya International Quality Summit Awards iliyofanyika nchini Marekani akiwapiku nchi 116 kutoka duniani kote.

Akizungumza na Globu ya Jamii katika maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Sabasaba, Mkurugenzi Mtendaji Dr Elizabeth amesema kuwa ameweza kufanikiwa kupata tuzo hiyo kwa sababu alibuni na kuthubutu kutengeneza vipodozi akiwa hajanakili au kukopi kutoka kwa mtu yoyote na zaidi amekuwa anatumia vitu vya kiasili kuvitengengeza.

Dr Elizabeth amesema kupitia kampuni yake ya Grace Natural Products ametengenza vipodozi bora na vimewasaidia watu wengi sana hususani wale waliotumia bidhaa za kemikali (sumu) na watakapoanza kutumia bidhaa zake huwasaidia kwa asilimia kubwa.

Amesema, moja ya sababu iliyoweza kumpatia tuzo hiyo ni namna alivyoweza kutengeneza vipodozi vya kiasili kwa ajili ya walemavu wa ngozi (albinism) na vimekuwa msaada mkubwa sana kwa matumizi yao ya ngozi kwakuwa na vimekuwa vikiuzwa kwa bei nafuu zaidi huku zikipata mjini na vijijini.

Dr Elizabeth ameeleza kuwa vipodozi vyake anatengeneza kwa kutumia mazao ya nyuki, matunda na mafuta ya asili ambayo hayana madhara kwa ngozi ya mtu yoyote bali itamfanya mtumiaji kuwa na ngozi nzuri na kuvutia.

Akizungumzia muitikio wa wananchi kwenye maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba kwa mwaka huu yamekuwa sio mkubwa sana tofauti na miaka mingine ila ameweza kupokea pongezi mbalimbali kutoka kwa watanzania waliofika kwenye banda lake.

Grace Product iliyoanza kazi miaka 10 iliyopita imeweza kuleta ushindani mkubwa katika soko la vipodozi na kufanikiwa kuwavutia watu wengi katika matumizi akiwa anatengeneza mafuta ya watoto, mafuta ya nywele, sabuni za kuogea, dawa za kusafishia choo pamoja na Shampoo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Grace Natural Products Dr Elizabeth Kalili akionesha tuzo yake ya The International Quality Summit Awards katika banda lake kwenye maonyelakeya 42 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Grace Natural Products Dr Elizabeth Kalili akiwaonyesha bidhaa kwa wateja waliojitokeza katika banda lake lililopo ndani ya Jengo la Sabasaba Hall kwenye maonyelakeya 42 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad