HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 7 July 2018

WATANZANIA WATAKIWA KUNUNUA VIFAA VYA UMEME VYENYE UBORA KUEPUKA MAAFA

Na Agness Francis, Globu ya Jamii.
Watanzania wametakiwa kutumia vifaa vya umeme vyenye ubora ili kuepukana na kuunguza vitu vyao kutokana na kutokuwa na ubora unaotakiwa kwa matumizi ya nyumbani au viwandani.

Hayo yamesemwa na Meneja Masoko wa Tropical Power Tanzania Rigobert Manega wakati wa maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam na kusema kuwa kwa mwaka huu wamewaletea watanzania transfoma zenye ubora wa hali ya juu kwa matumizi ya majumbani, viwandani na sehemu zingine mbalimbali.

Manega amesema kuwa muitikio wa wananchi kwa mwaka huu umekuwa ni mzuri sana na wengi wakionekana kuanza kuamini vitu vinavyotengenezwa nyumbani.

Amesema  wamekuwa wanatoa ushauri kwa watu binafsi, makampuni hata taasisi za kiserikali pindi wanapohitaji vifaa vya umeme ili kuendana na mahitaji yake.

Ameeleza kuwa kwa sasa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) wamekuwa wateja wao wazuri kutokana na ubora wa vifaa vya umeme wanavyovitengeneza hapa hapa nchini vikiwa na ubora wa hali ya juu.

Manega amesema kuwa, kwa sasa vifaa vyao vinauzwa ndani na nje ya nchi na mteja kabla ya kununia kifaa mtaalamu wao anaenda katika jengo, hotel au kiwanda kwa ajili ya kuangalia ni aina gani ya Transfoma inahitajika ili iweze kufanya kazi kwa ustadi unaotakiwa.


Baadhi ya bidhaa zingine wanazoziuza ni pamoja na waya za umeme mkubwa HTna LV, cables za umeme, waya za wiring za majumbani, PVC na vifaa vingine vya umeme.
Meneja Masoko wa Tropical Power Tanzania Rigobert Magena akizungumza na Globu ya Jamii na kuelezea umuhimu wa watanzania kutumia vifaa vyenye ubora na vinavyozalishwa ndani ya Tanzania kwenye Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Sabasaba Jijini Dar.
Meneja Masoko wa Tropical Power Tanzania Rigobert Magena akionyesha moja ya Transfoma wanayotengenza katika Kiwanda chao na zinatumika kwa matumizi mbalimbali nchini na nje ya Tanzania  kwenye Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Sabasaba Jijini Dar.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad