HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 3 July 2018

ULEGA ATEMBELEA FAMILIA ZA WAHANGA WA AJALI MKURANGA

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MBUNGE wa Mkuranga na Naibu Waziri wa mifugo na uvuvi Abdallah Ulega ametembelea familia zilizopatwa na msiba kutokana na ajali iliyotokea  mwezi uliopita huko Mkuranga.

Akizungumza na vyombo vya habari Ulega ameelezwa kusikitishwa na vifo vya watu 14 na majeruhi 4 ambao wamepoteza nguvu kazi, yatima, wajane na wagane.

Aidha Ulega amemshukuru Rais Magufuli kwa salamu zake za rambirambi ambazo ziliwasilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, pia amemshukuru Mkuu wa Wilaya na wajumbe wa CCM kwa ushirikiano wao katika hali mbalimbali.

Ulega amemtaka kamanda wa polisi kuangalia nidhamu kwa madereva wote hasa madereva wa malori ya mchanga ambao wameonekana kuwa na nidhamu ndogo barabarani.

Ulega aliwashika mkono wa pole katika vijiji 4 ambavyo ni Mlamleni kulikopata misiba 2, Mwanambaya msiba 1, Mkuranga misiba 5 na Tengelea misiba 8.
 Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega akizungumza nawafiwa wa ajali iliyo tokea mwenzi uliopita mwaka huu.(picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)

 Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega  akiwa na viongozi wa wilaya katika dua ya kuwaombea marehemu amabao walifariki katika ajali ya mwezi uliopita mwaka huu.

Naibu Waziri wa Mifungo na Uvuvi na Mbunge wa Mkuranga,Abdallah Ulega akisalimiana na wafiwa wa ajali iliyo tokea mwenzi uliopita mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad