HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 3 July 2018

SABASABA YAJA NA FURSA YA KUINUA VIJANA KIUCHUMI-VHV

Na Leandra Gabriel, blogu ya jamii

TAASISI ya House Of Vision (VHV)  inayojihusisha na ujasiriamali imejizatiti kutumia msimu huu wa sabasaba kuwasaidia vijana kutengeneza uchumi wao binafsi kutokana na ujuzi unaotolewa na taasisi hiyo.

Akizungumza na Michuzi Blog Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo bi. Zena Mulokozi ameeleza kuwa taasisi hiyo inatoa elimu ya ujasiriamali, ufugaji, mafunzo ya biashara na kujiajiri sambamba na utoaji mkopo wa fedha taslimu na vitendea kazi.

Bi. Zena emeeleza kuwa vifaa vitolewavyo kwa wanachama kama mkopo ni pamoja na pikipiki, mashine ya juice za miwa, bajaji, viwanja na mashamba.

Aidha ameeleza kuwa taasisi hiyo inatoa mafunzo ya ufugaji wa kuku wa kienyeji na kisasa.

Katika maadhimisho haya ya sabasaba  bi. Zena amewaomba vijana na watu wa kada mbalimbali kutumia fursa hii kujisajiri kwa vikundi kuanzia watu 15 hadi 30 na kusajiliwa katika banda lao.
Mkurugenzi wa taasisi ya  ujasiriamali ya House of vision  bi. Zena Mulokozi akizungumza na Michuzi Blog kuhusiana na fursa za ujasiriamali kwa vijana.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad