HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 24 July 2018

SINGIDA UNITED YAENDELEA KUIPIGA TAFU YANGA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Uongozi wa klabu ya Singida United kupitia kwa Rais wake Dkt Mwigulu Nchemba imeendelea kuipiga tafu timu ya Yanga baada ya kuwapatia mchezaji mwingine wa kigeni raia wa Zimbabwe.

Huyu anakuwa ni mchezaji wa pili baada ya Jana kuweka wazi kuwa Kiungo kutoka JKU Feisal Abdala 'Fei toto' kuwa wamemruhusu kwenda kukipiga katika klabu ya wanajangwani hao ikiwa ni moja ya mchango wake wa kuisaidia Yanga.

Ikiwa imepita siku moja toka kuweka wazi hilo, leo Uongozi wa Singida umetuma baru Katibu Mkuu wa Yanga na nakala nyingine kwa TFF na Bodi ya ligi kuwapa taarifa kuwa mchezaji Elisha Moroiwa kuanzia sasa ni mali ya Yanga.

Barua hiyo iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Singida United   AbdulRahman Sima imeweka wazi kuwa mchezaji huyo tayari ameshapatiwa fedha zake zote na hadai mkataba wowotena lengo kuu ni kuisaidia Yanga.

Yanga ambayo ipo katika kipindi kigumu wakiwa wanaandamwa na ukata wa fedha pamoja na viongozi kujiuzulu mpaka sasa walikuwa wameshafanya usajili wa wachezaji wanne wakimrejesha Mrisho Ngasa na Deus Kaseke ambao awali walikuwa wanacheza kwenye timu hiyo.

Takribani wachezaji saba ndiyo waliokuwa na mikataba huku wengine wakiwa wanataka kuongezewa mikataba na dirisha la usajili linatarajiwa kufungwa Julai 26 saa 6 usiku huku TFF wakisistiza hakutakuwa na muda wa nyongeza katika suala hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad