HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 24 July 2018

UZINDUZI WA SHOWTIME ENTERTAINMENT KUFANYIKA NGOME KONGWE MJINI ZANZIBAR

MKURUGENZI wa Kampuni ya Showtime Intertiment Ibrahim Mitawi amesema kuwa wanatarajia kuzindua  Kampuni yao ifikapo tarehe 27 mwezi wa saba mwaka huu katika Ukumbi wa Ngome Kogwe Zanzibar.

Hayo aliyasema huko katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar wakati akizungumza na Waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa Kampuni ya Showtime Intertiment inayotarajiwa kuanza saa moja Usiku.

Alisema kuwa lengo kuu la uzinduzi wa Kampuni hiyo ni kutaka kuijuilisha  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Wananchi kwamba Vijana wa Kampuni ya showtime wanauwezo mkubwa wa kuitangza Zanzibar kiusanii .

Aidha alisema kuwa Zanzibar ni Kisiwa cha Utalii hivyo watahakikisha kupitia Kampuni yao kwa kutumia vipaji walivyonavyo kuhakikisha wanaitangaza Zanzibar kupitia Matamasha mbali mbali ili  kuimarisha Utalii utaoengeza uchumi wa Nchi.

Hata hivyo alisema kuwa hawatoweza kuacha Utamaduni wao hivyo katika ufunguzi wa Kampuni hiyo kutakuwepo burudani mbali mbali za Utamaduni wa asili. 

Hata hivyo Ibrahim Mitawi alisema ili Sanaa ifike mbali zaidi kuutangaza Utalii  ni muhimu kuwepo na  mashirikiano baina ya Makampuni mbali mbali pamoja na Serikali.

 “Tunaomba mashirikiano yaendelee zaidi kati yetu kwani kufanya hivyo itapelekea Sanaa ya Zanzibar kufika Kimataifa na kupata fursa zaidi ya kuimarisha Utamaduni wetu utaopelekea kupata Watalii kutoka sehemu mbali mbali kuweza kuona utamaduni wetu”aliongeza zaidi Ibrahim Mitawi.

Pia alisema kuwa Kampuni yao inalengo la kuikuza Sanaa ya Zanzibar kufikia Kimataifa ili kuonyesha Vijana kuwa wanaweza na kuisaidia Serikali katika Suala zima la ajira kwa vijana ambao wanauwezo wa kuvitumia vipaji vyao kwa kujiajiri wenyewe.

“Sisi Vijana tumeamua kujiajiri wenyewe na kuanzisha Kampuni yetu ya Showtime Intertiment ili kuepuka kutegemea ajira kutoka serikalini “ alisema Mkurugenzi huyo.

Mkurugenzi huyo pia aliiomba Serikali kupunguza kodi ndogo ndogo wakati wanapoandaa matamasha mbali mbali ili kuweza kupunguza gharama kubwa ambayo hujitokeza kutokana na kodi hizo jambao ambalo linawakwamisha vijana hao ambao lengo lao ni kuingizia kipato serikali yao .

Akieleza zaidi alisema katika Tamasha hilo watakuwepo wageni mbali mbali kutoka Zanzibar na Nnje ya Zanzibar pamoja na Viongozi wa Serikali, Wakurugenzi  na Mameneja wa Mahoteli.

Nae Msemaji Mkuu wa Kampuni ya Showtime Intertiment Muslim Nassor alisema kuwa wapo tayari kufanya kazi na Kikundi chochote ambacho kitaweza kufanya Kampuni yao kufikia malengo waliyokusudia.

Akiongeza zaidi Muslim alisema kuwa wanaishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mashirikiano waliyowapa na kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi ili  kutimiza lengo la ufunguzi huo.

“Tunapenda kutoa shukurani za dhati kwa Serikali ya Mapindizi ya Zanzibar na Wananchi tunawaomba kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia uzinduzi huo  wa Kimataifa ambao haujawahi kutokea.

Sambamba  na hayo alisema Kampuni ya Showtime Intertiment ni kampuni inayojihusisha na masuala ya uandaaji wa shughuli mbali mbali za kitaifa na Kimataifa kama vile Matamasha , kufanya Matangazo na ukodishaji wa Vifaa vya Muziki na Majukwaa.

Kampuni ya Showtime Intertiment imeanzishwa miaka miwili (2) iliyopita na ina idadi ya watu 45 ambao wamejitolea katika Kampuni hiyo.
 Msemaji wa  Showtime Intertinment Musilim Nassor akizungumza na Waandishi wa Habari hawapo pichani juu ya Uzinduzi wa Showtime itakayozinduliwa tarehe 27/07 2018 katika Ukumbi wa Ngome Kongwe Mjini Zanzibar.
 Mkurugenzi wa Showtime Intertinment Ibrahim Mitawi akitoa ufafanizi  wa masuali aliyokua akiulizwa na Waandishi juu ya Uzinduzi wa Showtime  hiyo itakayozinduliwa tarehe 27/07 2018 katika Ukumbi wa Ngome Kongwe Mjini Zanzibar (kushoto) ni Saleh Nassor Abdallah ( Dj CARTEL) na Msaidizi Itifaki Issam Ramadhan Mussa.
  Mwandishi wa Habari wa Gaziti la Majira Mwajuma Juma akiuliza maswali katika mkutano kuhusiana na Show hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa tarehe 27/07/2018  katika Ukumbi wa Ngome Kongwe Mjini Zanzibar.
Msaidizi Itifaki Issam Ramadhan Mussa akijibu baadhi ya maswali yaliokua yakiulizwa na Waandishi kuhusiana na Show hiyo (kulia) ni Dj CARTEL, Mkurugenzi wa Showtime Intertinment Ibrahim Mitawi na Msemaji wa Taasisi hiyo Musilim Nassor.
Picha na Abdalla Omar  Maelezo – Zanzibar.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad